Wakazi wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha, wakimsikiliza mbunge wa
Arusha Mjini kupitia Chadema, Godbless Lema alipohutubia mkutano wa
hadhara kulaani kuadimika kwa mafuta ya petroli na mgao wa umeme
unaondelea nchini, mkutano ulioambatana na ufunguaji wa matawi ya Chama
hicho. Picha na Silvan Kiwale
--
SHUGHULI
mbalimbali zikiwamo za kiuchumi na kijamii katika baadhi ya mitaa ya
jiji la Arusha, jana zilisimama kwa muda wakati misafara mirefu iliyojaa
mbwembwe za kila aina ya magari, pikipiki, baiskeli na mikokoteni
iliyofungwa bendera za Chadema, ilipopita kwenye kata nne ambazo
zilikuwa zikiongozwa na madiwani kiliowatimua uanachama hivi karibuni.
Ziara
hiyo ya kwanza ya viongozi wa juu wa Chadema imekuja siku chache baada
ya Kamati Kuu (CC) ya chama iliyokutana Mjini Dodoma kati ya Agosti 5 na
6, kuamua kuwafukuza uanachama madiwani wake watano kutokana na madai
ya kuingia muafaka na CCM na TLP katika nafasi ya umeya wa jiji hilo
Juni 20, mwaka huu bila ridhaa ya uongozi wa taifa.Kwa habari zaidi bofya na Endelea....>>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)