Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa
mwitu Mkurugenzi wa shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi
kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa utunzwaji wa mbwa mwitu
katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Vodacom Foundation’s Serengeti
Wild Dogs Conservation Project).Mradi huo ulizinduliwa juzi na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige(katikati)ambapo Vodacom Foundation
imetoa dola za Kimarekani 450,000 kwa miaka mitatu.
Waziri
wa wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akijadiliana kuhusiana na
masuala ya uhifadhi na utalii na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom
Tanzania Dietlof Mare,kabla ya uzinduzi rasmi wa mradi wa (Vodacom
Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project)Kulia ni mjumbe wa
bodi ya wadhamini ya Vodafone Foundation toka nchini Uingereza,Bi
Elizabeth Filkin.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, wakifurahia jambo na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, baada ya kuwasili kwenye kambi ya
utalii ya Soroi, Serengeti kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi
mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation
Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare(kulia)akimuonyesha kitu Afisa
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bi Mwamvita Makamba
kwenye kambi ya utalii ya Soroi, Serengeti wakati wa uzinduzi wa mradi
wa kuhifadhi mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs
Conservation Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
--------
Na Mwandishi wetu,Serengeti.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige,juzi amezindua mradi wa uhifadhi
Mbwa Mwitu ujulikanao kama “Vodacom Foundation Serengeti Serengeti Wild Dogs Conservation Project” katika
hifadhi ya taifa ya Serengeti,mradi ambao unafadhiliwa na kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom kwa kiasi cha dola zakimarekani 450,000 kwa
miaka mitatu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Mradi huo,Waziri Maige alisema Mbwa mwitu ni
miongoni mwa wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka duniani hivyo
jitihada kubwa zinahitajika kuwalinda na kuwahifadhi.Waziri Maige
alisema katika bara la Afrika kuna idadi ya Mbwamwitu, wanaofikia 8000
na Tanzania pekee ina jumla ya mbwamwitu 3500 ambao wapo hatarini
kutoweka hivi sasa.
Alisema
katika hifadhi ya Serengeti makundi ya Mbwamitu ambayo yalikuwa
yanaonekana sasa yametoweka na mara ya mwisho mbwamwitu wawili tu
walionekana mwaka 1998.
Waziri
Maige alisema, Mwa mwitu hao, wamekuwa wakitoweka kutokana na kuuwa na
wananchi baada ya kula mifugo yao, kuugua magonjwa mbali mbali
ikiwepo kichaa cha mbwa.
“napenda
kuwapongeza Vodacom kwa kujitokeza kudhamini uhifadhi wa mbwamwitu
kwani wanasaidia kuvutia watalii kuja Tanzania na hivyo kuongeza pato
la taifa”alisema Maige.
Alisema
sekta ya utalii nchini inachangia asilimia 17 ya pato la taifa hivyo
ni wajibu wa makampuni kusaidia sekta hii kwani imeajiri zaidi ya watu
700,000 ambao pia ni wateja wa kampuni mbali mbali.Awali Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare.alisema kampuni hiyo,
imeamua kujitokeza na kusaidia sekta ya utalii ili kuongeza pato la
taifa.
Alisema
Vodacom inaamini kuwa Tanzania ni nchi ya kipekee duniani katika sekta
ya utalii kutokana na kuwa na vivutio vingi na hivyo lazima vitunze na
kuhifadhiwa.
“vodacom
tumeamua kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano kusaidia sekta ya
utalii na tunaamini katika ufadhili wetu, mbwamwitu waliohatarini
kutoweka sasa watarejea hifadhi ya Serengeti”alisema Mare
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Utafiti wa
Wanyamapori,(TAWIRI) Dk.Simon Mduma alisema TAWIRI ambao ndio
wasimamizi wa mradi huo watahakikisha wanashirikisha jamii kuwalinda na
kuwahifadhi Mbwa mwitu.
Mduma
alisema katika siku za karibu makundi ya Mbwamwitu yamekuwa
yakionekana katika pori tengefu la Lolindo na vijiji vya Tarafa ya sale
ikiwepo Samunge na tayari umewekwa utaratibu wa kuwafuatilia na
kuwalinda.
MWISHO.








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)