Viongozi sita wa madhehebu ya dini wanaojihusisha na biashara haramu ya
dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya
Viongozi wa Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo
kwa muda mrefu sasa.
Afisa
Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema
kuwa baada ya kuhojiwa, Viongozi hao waliiomba Kamati hiyo kutowataja
hadharani majina ama madhehebu yao kwa kuhofia kubezwa kwa madhehebu
wanayoyaongoza.
Akizungumza
mwishoni mwa ziara yao Visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, amesema
kuwa orodha hiyo na nyingine ya watu 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa
na Wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu zote zitafikishwa
kwa Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Kupambana na dawa za Kulevya nchi.
Mchungaji
Mwamalanga amesema kuwa, tatizo la ongezeko la dawa za kulevya pia
inazihusu nchi mbalimbali duniani na kwamba kamati hiyo itakutana na
kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kwa maana ya Afrika ya
Mashariki kuzungumzia ufumbuzi wa suala hilo.
Amesema
mkutano huo pia utapendekeza kwa mabunge ya nchi hizo na Bunge la
Afrika ya Mashariki kutunga sheria za kuwafilisi wale wote
waliojilimbikizia mali kutokana na biasha za dawa za kulevya kwa nchi
wanachama.
Hata
hivyo Kamati hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii ikiwa
hapa Visiwani, imesifu na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kwa hatua
zao za kukabiliana na ongezeko la dawa za kulevya.
Akizungumzia
kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini
Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa Jeshi hilo
limekuwa likiwakamata wengi wa wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za
kulevya na kuwafikisha mahakamani.
Hata
hivyo, kamanda Aziz ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa
usalama kuendelea kusaidiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale
wote wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.
Kamanda
Aziz amesema kama kila mwananchi atatoa taarifa za siri Polisi za
kuwepo kwa mtu ama kundi la watu wanaojihusisha na biashara hiyo ama
uhalifu mwingine wowote, ni wazi kabisa kuwa Polisi iyawatia mbaroni.
Wiki
iliyopita watu wawili wakazi wa Jijini Dar es Salaam, wamekamatwa
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa nyakati tofauti
wakitokea nchini Brazil ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa
cha madawa ya Kulevya aina ya Cocaine.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)