Moja Ya Picha Za Wanafunzi Wakiandamana Katika Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa Na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Mnamo Tarehe 20 December 2010
...................................................
Baadhi ya Wabunge wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina kuhusu migomo ya mara kwa mara katika chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kusababisha chuo hicho kichanga kuonekana ni kinara wa migomo hiyo nchini.
Wamesema kuwa Serikali inatakiwa kuchunguza kwa kina ili kukomesha migomo hiyo katika vyuo mbalimbali nchini hususani Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kimeonekana kuwa kinara wa migomo hiyo.
Wamesema kuwa Serikali inatakiwa kuchunguza kwa kina ili kukomesha migomo hiyo katika vyuo mbalimbali nchini hususani Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kimeonekana kuwa kinara wa migomo hiyo.
Pia wamewataka baadhi ya wanasiasa kuacha tabia ya kueneza siasa katika chuo hicho kufuatia kusadikika kuwa huchangia migomo ambayo haina tija kwa wanafunzi na Taifa kwa ujumla.
Wabunge hao wameyasema hayo wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012 mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)