Katibu
Mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii bi. Blandina Nyoni,akisoma
hotuba kwenye semina ya wabunge kuhusu majukumu ya bohari kuu ya madawa
nchini.
Mkurugenzi
wa Ununuzi na Shughuli za kitaalam bi. Lucy Nderimo akitoa mada
iliyohusu mfumo wa ugavi wa bohari kuu ya dawa ambapo manunuzi yote
yanafanyika kwa kuzingatia sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni
zake za mwaka 2005.
Mkurugenzi
wa mahusianao ya wateja na uendeshaji wa kanda toka msd, bw. Cosmas
Mwaifani akitoa mada iliyohusu miaka 17 ya MSD,ufanisi na changamoto
(1994-2011).Alitaja changamoto zinazoikabili bohari hiyo ni pamoja na
ile ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vya umma kwenye maduka na
vituo vya afya vya watu binafsi na uchache wa viwanda vya ndani katika
sekta ya uzalishaji dawa na vifaa tiba ambao unakidhi mahitaji ya nchi
kwa asilimia 20 tu.Picha na Mdau Cathy Sungura-MOH
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)