Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa katika foleni ya
kujiandikisha upya na kupatiwa vitambulisho vipya pamoja na namba za
kurejea chuoni baada ya wanafunzi hao kuanza kurejea chuoni.
Wanafunzi hao waliandaliwa utaratibu wa kujiandikisha upya ikiwa ni
pamoja na kuhakikiwa kuhusu malipo ya Ada, pamoja na kuapishwa na
Wanasheeria wakiapa kuwa hawatarudia tena kugoma.
Askari Polisi
akienda kwa baadhi ya wanafunzi ili kuwaelekeza kukaa katika foleni na wasiweze
kuchakachua na kurukia foleni za wenzao wakati wa mchakato huo,
ulifanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
"Duh! Tumewahi Kuamka Saa 11 Alfajili Na Namba Tumekosa....?" Baadhi ya Wanafuzi waliochelewa kuchukua namba ya kuingia kwenye usaili huo,wakichungulia kwenye moja ya mageti ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Hawa ndo kwanza wamejichokea kusubiri utaratibu wa kuitwa ili kuanza hatua ya mwanzo ya ukaguzi wa Ada.
Wengine waliochelewa kuchukua namba wakiwa nje ya geti kuu la kuingilia kusubiria taratibu ya viongozi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)