Picha
juu ni za Timu ya wakongwe wa muziki wa dansi Wakijisua kisawasawa kwa
ajili ya Tamasha la Sauti za Kale litakalofanyia leo jijini Dar es
Salaam
--
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAMASHA LA SAUTI ZA KALE
21/07/2011
Timu
ya wakongwe wa muziki wa dansi nchini inayowakusanya wanamuziki akiwemo
Kingkikii, Mafumu Bilali, Kasongo Mpinda, john Kitime, Abdul Salvador,
Babu Njenje, Mzee Waziri na wengineo, wanatarajia kufanya tamasha lao
ambalo hufanyika kila mwaka na safari hii liko njiani kuelekea kileleni
kwani linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Selander Bridge maeneo
ya Upanga tarehe 22 Julai 2011.
Lengo
la tamasha hilo ni kuhuisha uwepo wa wanamuziki wa zamani kwa
kudhihirisha kuwa uwezo wao kisanii bado uko juu, halikadhalika mchango
wao katika kudumisha sanaa ya muziki wa Tanzania upo pale pale na pia
kuikumbusha jamii kuwa walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.
Nia
yao nyingine, ni kuweka daraja baina ya wanamuziki wakongwe na wasasa
ili kutengeneza muendelezo mzuri unaotokea kwenye chimbuko la muziki wa
kitanzania na kuwaonesha vijana wanaochipukia kisanii kuwa muziki
umetoka wapi, unaenda wapi na umefika wapi.
Siku
hiyo inatarijiwa kuwa ni siku ya aina yake kwani wakongwe hao
wanatarajia kutambulisha wimbo wao mmoja na mpya kati ya nyimbo tatu
walizorekodi, na wimbo huo unajulikana kwa jina la Tanzania, wakiwa wame
urudia katika midundo ya kisasa,kwani wenyewe ulipigwa na Atomic Jazz
Band chini ya utunzi wake Steven Hiza mnamo mwaka 1965.
Wakongwe
hao wameshakamilisha nyimbo zao tatu ikiwepo hiyo Tanzania, Miaka
Hamsini ya uhuru pamoja na Kilimo kwanza na zote hizo chini ya usimamizi
wake Prodyuza Allan Mapigo wa Metro Studio.
Kwa kuwapa Saport wakongwe hao ni kuchangia kwa kiasi kikubwa kuuinua muziki wa watanzania.
Wote Mnakaribishwa
SAUTI ZA KALE.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)