Inspekta Jenerali wa Polisi
Said Alli Mwema
---
2. Mnamo tarehe
22/7/2011 Inspekta Jenerali wa Polisi Said Alli Mwema alitoa wito kwa wananchi
wote kupitia vyombo vya habari kuwa, katika utekelezaji wa kampeni ya kutii
sheria bila kushurutishwa wale wote wanaomiliki silaha isivyohalali
wazisalimishe kwa hiari na zinazomilikiwa kihalali zihakikiwe upya.Na zoezi hili
ni kwa muda wa miezi mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Octoba
31,2011.Katika kipindi hicho hakutakuwa na hatua zozote za kisheria
zitakazochukuliwa dhidi ya mtu atakayesalimisha/kuhakiki silaha kwa hiari
yake.
3.
Tunawashukuru wananchi ambao wameanza kuitikia wito huo kwa kuanza kusalimisha
silaha zao kwa hiari. Pamoja na hayo, inaonekana bado kuna makundi ya watu/watu
ambao bado wanaendelea kumiliki na kufanyia uhalifu silaha wanazozimiliki isivyo
halali.
4. Mfano wa matukio
hayo ni kama ifuatavyo, mnamo tarehe 28/7/2011 majira ya saa 7 usiku katika Mkoa
wa Kagera wilaya ya Biharamuro, wananchi wema walitoa taarifa polisi kuwa, kuna
majambazi yapatayo 6 katika eneo la pori lililopo kati bwanga na Bihalamuro
wamejipanga kuteka magari ya abiria/ mizigo yanayopita katika eneo hilo, baada
ya polisi kupata taarifa hizo, walienda katika eneo hilo na ghafla majambazi
hayo yalianza kuwafyatulia risasi. Katika kurushiana risasi Polisi walifanikiwa
kuyaua majambazi yote sita (6) na kufanikiwa kupata silaha 2 aina ya SMG na
risasi 180.
5. Aidha, katika
tukio jingine la kusikitisha mnamo tarehe 27/7/2011 majira ya usiku huko katika
kijiji cha Genkuru Tarime Rorya askari Polisi No.F. 4268 D/C Pendo
aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni na jambazi aitwae Bhoke Mohere waliyekuwa
wameenda kumkamata nyumbani kwake kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na
kumiliki silaha isivyo halali. Baada ya mauaji hayo jambazi hilo lilifanikiwa
kutoroka.
6. Hali hii,
inadhihirisha wazi ni jinsi gani askari polisi wanafanya kazi katika mazingira
hatarishi, pamoja na kwamba wanakuwa wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata
matakwa ya sheria, lakini kuna mahali wanakutana na mazingira ya watu wabaya
wanaokaidi kutii sheria,hali inayopelekea askari wenyewe kuuawa ama
kujeruhiwa.Na hii ina maana kwamba nguvu anayoitumia mhalifu katika kupambana na
askari ndiyo inayomlazimu askari Polisi kuona atumie nguvu kiasi gani ili aweze
kumdhibiti mhalifu huyo.
8. Wito wangu kwa
jamii, wakati zoezi hili linaendelea nawaomba wananchi wote waendelee kutoa
taarifa za watu wanaowafahamu ambao wanamiliki silaha isivyohalali ili kusaidia
kuwabaini endapo watakaidi agizo la kusalimisha silaha hizo kwa
hiyari.
Imeandaliwa na
Advera Senso- ASP
Msemaji Mkuu wa Jeshi la
Polisi
Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)