KIONGOZI wa timu ya Bunge iliyofuatilia hukumu ya malipo ya rada
ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Job Ndugai (katikati) akitoa taarifa ya ujumbe wa timu hiyo
katika ukumbi wa mikutano Bungeni mijini Dodoma. Kulia kwake ni mjumbe
wa timu Mhe. Angela Kairuki (Viti Maalum) na kushoto ni Mussa Azzan
Zungu (Ilala).
MJUMBE wa timu ya Wabunge la Bunge la Tanzania waliofuatilia
hukumu ya malipo ya rada kutoka kampuni ya BAE ya nchini Uingereza,
Mussa Azzan Zungu (Ilala) akitoa taarifa kwa waandishi wa
habari kuhusiana na mambo yaliyoajiri katika ziara hiyo
nchini Uingereza. Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika leo
(jana) Bungeni mjini Dodoma.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Anne Makinda akipokea ripoti ya timu ya wabunge wa Bunge
la Muungano wa Tanzania kutoka kwa Kiongozi wa timu hiyo ambaye ni
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai. Timu hiyo ilikwenda nchini
Uingereza kufuatilia hukumu ya malipo ya fedha za rada kutoka katika ya
British Aerospace (BAE ) ya nchi humo ambayo inadaiwa na Serikali ya
Tanzania kiasi cha zaidi ya Tsh. Bilioni 80. Mkutano huo na waandishi
wa habari umefanyika leo (jana) Bungeni mjini Dodoma.




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)