Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Makaburi ya naliendele mkoani Mtwara.
-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimia wananchi katika sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Mkuki, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea kukagua makaburi 101 kati ya 108, ya askari ‘Mashujaa’ walifariki wakati wakipigana vita Msumbiji na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara, wakati wa sherehe za kumbukumbu za Mashujaa zilizofanyika leo Julai 25, 2011 mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Balozi Seif Ali Idd, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa pili, Balozi Seif Ali Idd, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja hivyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigava Vita, ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya mashujaa iliyofanyika kwenye viwanja vya naliendele, Mkoani Mtwara leo Julai 25.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.Picha na Muhidini Sufiani -Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)