KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Magharibi Zanzibar Mjumbe Msuri Mjumbe (wan ne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa CCM wa wilaya hiyo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
 Naibu waziri wa Afya na Ustawi  wa Jamii Lucy Nkya (katikati), naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri (kulia) na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole-Nangoro (kushoto) wakijadili jambo leo wakati wa kikao cha bunge la  bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.
 Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika  Prof. Jummanne Maghembe akiwasoma bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
 Viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) wakifuatilia kwa umakini bajeti ya wizara ya  Kilimo,  Chakula na Ushirika  wakati waziri wa wizara hiyo Jummanne Maghembe (hayupo pichani) alipokuwa akiisoma leo  bungeni mjini Dodoma. TMF kupitia mpango wao wa fellowship kwa mwaka huu imefadhili waandishi wa habari watano kwa ajili ya kuandika habari za uchunguzi kuhusu masuala ya kilimo  vijijini kwa kipindi cha miezi sita.
 Mbunge wa Kilwa  Kusini kupitia  chama cha CUF Selemani Bungara akichangia hoja kuhusiana na masuala ya kilimo katika jimbo lake mara baada ya waziri wa wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Jummanne Maghembe (hayupo pichani) kuwasilisha bujeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma .
 Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi (kushoto)  akimsikiliza Naibu waziri wa Nishati na Madini Adam Malima (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha asubuhi cha maswali na majibu katika bunge la 10 la mkutano wa bajeti kikao cha thelathini na mbili kinachoendelea mjini Dodoma. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages