Ni
katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Monesho ya 35 YA Kimataifa
yanayoendelea, ndani ya Jengo la Karume, palipo na Banda la Idara ya
uhamiaji. Hapo utakutana na wahudumu wenye ujuzi, wanaoelekeza kwa
ufasaha na kutoa huduma za Visa, Passport, Visa ya muda mfupi, CTA na
huduma nyinginezo muhimu. Ukifika Bandani hapo,utahudumiwa na kujifunza
mengi yenye tija kwako na kwa Taifa Tanzania.
Msemaji
Msaidizi Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan, akitoa maelekezo na kumpatia
kipeperushi mwananchi aliyefika katika Banda la Uhamiaji ndani ya
jengo la Karume kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya
35 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Idara
ya Uhamiaji wana machapisho na vipeperushi vingi ambavyo huwapatia
wananchi wanaofika hapo wajisomee na kuelewa shughuli mbali mbali
zinazofanywa na Idara hiyo nyeti.
Afisa
wa Uhamiaji, Idara ya Uhamiaji, akimsikiliza kwa makini na kumuhudumia
mwananchi aliyefika bandani hapo kujaza fomu kwa ajiri ya kupata
Passport.
Afisa
Uhamiaji, Sophia Gunda, akimfafanulia jambo mwananchi aliyefika Banda
la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara,
sabasaba.
Raia
wa Kigeni akipata maelekezo sambamba na kuchukua vipeperushi katika
Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya
Bisahara, sabasaba. Picha zote na Victor Makinda.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)