3:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri
Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela, wakati
alipofika nyumbani kwake mjini Dodoma jana Julai 29,kmjulia hali baada
kufanyiwa upasuaji nchini India hivi karibuni. Kushoto ni Mama Asha
Bilal.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (kulia) akifurahia jambo na mke
wa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela,
wakati alipofika nyumbani kwake mjini Dodoma jana Julai 29,kmjulia hali
baada Malecela kurejea nchini kutoka kufanyiwa upasuaji nchini India
hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mke wa
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela (wa pili
kulia) ambaye pia anaagana na mke wa Kamau wa rais Mama Asha Bilal,
baada ya mazungumzo wakati walipofika nyumbani mstaafu huyo mjini Dodoma
jana Julai 29,kmjulia hali baada kufanyiwa upasuaji nchini India hivi
karibuni.
7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha
Bilal (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu na Makamu wa
kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela na mkewe,Anne Kilango, wakati
Makamu alipofika nyumbani kwa Malecela mjini Dodoma jana Julai 29, kwa
ajili ya kumjulia hali baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India hivi
karibuni. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)