Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wageni
waalikwa mbalimbali katika hafla ya kuburudisha ya wabunge na kutambulisha nembo
nyekundu na mpya ya kampuniya Vdacom Tanzania kwenye hafla hiyo iliyofanyika
usiku huu katika viwanja vya bunge mjini Dodoma, huku mgeni rasmi akiwa Waziri
mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Mizengo Pinda, FULLSHANGWEBLOG imetia
timu mjengoni kwa ajili ya kukumuvuzishia matukio usiku huu endelea kupata
uhondo kutoka viwanja vya bunge.
Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama
Anne Makinda akimkaribisha Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla
hiyo usiku huu.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisakata Rhumba na Spika
wa bunge Mh Anne Makinda katika hafla ya kuburudisha wabunge iliyoandal;iwa na
kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya
Bunge mjini Dodoma.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akicheza
muziki na mmoja wa wabunge bwa bunge la Jamhuri yaq muungano wa Tanzania katika
hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania.
Aliyewahi kuwa mshiriki wa Tusker Project Fame ambaye
pia ni mwimbaji wa bendi ya B. Band Annet Kashaba akiimba katika hafla hiyo.
Mbunge wa Tabora mjini Mh. Aden Rage
akicheza na Naibu waziri wa Jinsia wanawake na watoto Mh. Ummy Mwalimu.
Waziri
Mkuu wa Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vodacom
Tanzania Dietlof Mare, wakati alipokuwa akiwasili katika hafla ya kuwaburudisha
wabunge na kuitambulisha rasmi nembo nyekundu ya kampuni ya Vodacom,
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Anne Makinda kulia, na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania
Dietlof Mare mara baada ya kumpokea Mgeni Waziri mkuu.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda wa pili kushoto akiwasili katika hafla iliyoandaliwa na
kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, kwa ajili ya kuburudisha wabunge
jioni hii katika viwanja vya bunge.
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akisalimiana na Kiongozi wa upinzani bungeni
Mh. Freeman Mbowe katika sherehe hiyo.
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akisalimiana na Kiongozi wa upinzani bungeni
Mh. Freeman Mbowe katika sherehe hiyo.
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare kulia akizunguza jambo na Spika wa bunge Mh
Anne Makinda, katikati ni Mwamvita Makamba Afisa mkuu wa Masoko na Mahusiano wa
Vodacom Tanzania.
Spika
wa Bunge Mama Anne Makinda akifurahia jambo na Waziri ofisi ya Waziri mkuu sera
uratibu na bunge William Lukuvi, katikati ni Mh. Simbachawene.
Wanamuziki
wa muziki wa taarab Shakira kushoto na Patricia Hillary wakiimba katika hafla
hiyo.
Mwanamuziki
Banana Zoro akifanya vitu vyake jukwaani katika hafla ya kuwaburudisha wabunge,
iliyoandaliwa na kampuni simu za mkononi ya Vodacom Tanzania inayofanyika usiku
huu katika viwanja vya Bunge. 












No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)