FREDY MPENDAZOE AFANYA MKUTANO WA HADHARA TABATA LIWITI KATA YA SEGERA JIONI YA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

FREDY MPENDAZOE AFANYA MKUTANO WA HADHARA TABATA LIWITI KATA YA SEGERA JIONI YA LEO

Moja Ya Gari la Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) Yanayotumika katika Kampeni Za Chadema na Operesheni Zao likiwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Liwiti Tayari Kwa Viongozi Wa Chadema Kupanda Jukwaani Kuwahutubia Wananchi Wa Segerea Na Vitongoji Vyake
Diwani Wa Kata Ya Segerea Mh Azuhuri Mwambagi Akiwahutubia Wananchi Juu Ya Kazi Alizoweza Kuzifanya Mpaka Sasa tokea Alipochaguliwa Kuwa Diwani Wa Kata Hiyo leo Jioni katika Viwanja vya Shule ya Msingi Liwiti Tabata Segerea
Mh Diwani Wa Kata Ya Segerea Azuhuri Mwambagi Akiwaeleza Wananchi Juu Ya Hali Ya Kisiasa Nchini Pamoja na Tatizo la Umeme Tanzania
Wananchi wa Kata ya Segerea na Vitongoji Vyake walivyojitokeza kwa wingi kusikiliza mkutano huo wa Chadema uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Liwiti Tabata Segerea Jioni Ya leo
Wananchi Wakiwa Makini Kusikiliza Kinachohutubiwa Na Viongozi Wa Chadema Katika Mkutano huo
Viongozi Wa Chadema Wa Jimbo la Segerea Na Kutoka Makao Makuu Ya Chadema Wakiongozwa Na Mh Fred Mpendazoe Wakiimba Wimbo Wa Tanzania Tanzania Huku Maneno Ya Kiitiko Wakisema CCM na Wananchi Wakiitikia Kwa Kushika Vichwa
Wananchi Wakishika Kichwa Kama Ishara Ya Kiitiko Kilichokuwa Kikisemwa na Fred Mpendazoe. Fred Mpendazoe Akisema "CCM OYEEE majibu ya wananchi Ni Kushika Kichwa Na Kusema aaaaahhhhhhhh''
Fred Mpendazoe Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Segerea Akielezea Wananchi Jinsi Kesi Yake Dhidi Ya Mh Mahanga Kuhusu Matokeo Ya Uchaguzi Uliofanyika 31/10/2010 inavyoendelea na kwamba Kesi hiyo itaendelea tena tarehe 27 mwezi huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Kijana Mdogo Kabisa Akiwa Anakatiza Mbele ya Kamera Ya Lukaza Blog Akiwa Amevalia Kofia Ya CHADEMA katika mkutano huo uliofanyika Jioni Ya Leo katika Uwanja wa shule ya msingi Liwiti Tabata Segerea
 Hapa ilikua ikisemwa Salamu Ya Chadema.....CHADEMAAAAAA wananchi walikua wakiitikia Kwa Kukunya Ngumi Na Kusema Vyemaaaaaaaaaaa.
Mzee Mmoja Ambaye Jina Lake Halikuweza Kupatikana Mara Moja(mwenye suti) Alikua Akisema CCM oyeee wakati Wa Mkutano Wa Chadema Ukiendelea Jioni Ya Leo Huku Vijana Wa Chadema wakimzuia na Kumtaka Aondoke Ili kuepusha Vurugu. Zengwe liliendelea Hivi.....
Alipoanza Safari ya Kuondoka Kukwepa Kipigo ambacho akipata kutoka Kwa Vijana Hao wa chadema huku akiwachimba mkwara vijana hao
Akiendelea Kuwachimba Biti Vijana Waliokuwa Wakimzomea Huku Mdogomdogo akitoweka kufuta aibu hiyo.
Mzee Huyo akitaka Kuvuka Barabara Huku Mapapari Wakichukua Taswira Zake kwa kwenda mbele
Wananchi Wakiitikia Salamu Ya Chadema Huku Wakinyoosha Ngumi Juu. Picha Zote Na Mpiga Picha Maalumu Wa LUKAZA BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages