Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezikana nyaraka za siri
zilizodaiwa kunaswa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kuwa si zake na hazikuandikwa na chama
hicho.
Katibu
Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, alitoa ufafanuzi huo alipokuwa
akizungumza na NIPASHE kuhusiana na taarifa zilizoandikwa juzi na gazeti
dada la NIPASHE JUMAPILI likimunukuu Nnauye kuwa amenasa nyaraka za
Chadema zilizokuwa zikitoa maelekezo kwa viongozi wa chama hicho wa
ngazi ya mikoa na majimbo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi,
Nape alisema nyaraka alizonasa ni pamoja na barua yenye kumbukumbu namba
CDM/DSM/HU/Vol 040/2011 ya Julai 20, 2011 iliyosambazwa kwa wenyeviti
wa kila mkoa kuandaa maandamano nchi nzima baada ya Mkutano wa Bunge la
bajeti.
Alisema
barua hiyo iliyokuwa imesainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
Chadema, Erasto Tumbo, ilikuwa ikiwashinikiza wenyeviti kuandaa
maandamano hayo kwa nia ya kuiabisha serikali kwa madai kwamba
imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha
alisema kwamba aliinasa barua nyingine ya Chadema yenye kumbukumbu
namba CDM/DSM/Vol.138/2011 ya Juni 30, 2011 iliyosainiwa na Tumbo kwenda
kwa makatibu wa majimbo kutekeleza agizo la Dk. Slaa la kuwahamasisha
wananchi wagomee shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Dk.
Slaa alisema mfumo wa namba za kumbukumbu katika barua zote mbili
zilizotolewa na Nnauye kwenye mkutano huo, haziendani na mfumo wa kuweka
namba za kumbukumbu unaotumiwa na Chadema.
“Mbali
na dosari hiyo iliyoko kwenye barua za Nnauye, hata katika tarehe
ambazo Nnauye anadai kwamba barua hizo ziliandikwa yaani, Julai 20, 2011
na Juni 30, 2011, hakuna barua yoyote iliyoandikwa toka au kuingia
makao makuu ya Chadema,” alisema. Dk.
Slaa alisema yeye binafsi na Chadema kwa ujumla, wanafahamika na
wananchi jinsi walivyomstari wa mbele kuhamasisha maendeleo ya wananchi,
kwa hivyo haiwezekani wakashiriki kwa namna yoyote ile kuwazuia
wananchi wasichangie maendeleo.
Dk.
Slaa alisema suala la maandamano kwa Chadema halihitaji kuandikiwa
waraka wa siri hata siku moja kwa kuwa wao hutangaza hadharani
wanapohitaji kufanya maandamano.
“Chadema
huwa tunatangaza maandamano yetu hadharani, mbele ya vyombo vya habari,
kupitia kwenye mikutano tunayofanya. Tumeshasema kwamba tutaendelea
kuandamana mpaka kieleweke na watu wote wanatambua hilo,” alisema na
kuongeza: “Sasa kwa nini tuandike barua ya siri? “Alisema
bado wananchi wanakabiliwa na maisha magumu,ufisadi, tatizo la umeme
nchini na bei ya vyakula kuendelea kupanda, Chadema wataendelea
kuandamana na safari hii maandamano yao yatakuwa katika mikoa ya Dodoma,
Singida, Morogoro, Manyara na Tabora.
Dr Slaa na Chadema waulizwe, maandamano ndio suluhisho la ugumu wa maisha, ufisadi, tatizo la umeme na bei la vya kula kupanda bei? Tatizo mchungaji Dr Slaa anapenda kuchukua short cuts, hatumii proper channels, kumpata mke, kaona bora kuchukua mke wa mtu, hahitaji grooming well experienced!
ReplyDeleteNia yake ni ku-distablize serekali kama vile alivyojaribu ku-distabilize the catholic church by marrying, remember this is his first wife Mary Kamili......ambae hatajwi kabisa lakini ni mama wa watoto wake but she too has been bought and paid for by Chadema she dares not speak about her rights....mie nashanga hata hizi NGO's zinazodai kukomboa wanawake hawaoni hili...uzushi mtupu.
Sasa anataka kuwavunga wananchi badala ya kufanya shughuli za maendeleo wakaandamane. akumbuke hata kama atapata fursa ya kuogoza matatizo haya hayata isha kwa siku 90/100 kama wanavyodai kwa hiyo maandamano hayata komea hapo.....je anataka nchi yetu ya amani iwe ya maandamano tu? Mchungaji utawaweka pabaya kondoo wako. Muogope mungu, usiwemnafiki wa nafsi.