Baadhi ya Wanafunzi waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu ambao unaendelea kufanyika katika kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha
Daktari wa Zahanati ya Chuo Kikuu Cha Dodoma akimtoa damu mmoja wa wanafunzi hao waliojitokeza katika zoezi hilo mchana huu.
Wanafunzi Wa UDOM akiwepo na Mama Kazoba (anayetabasamu) wakiwa kwenye viti maalumu kwa ajili ya kutolewa damu mchana huu katika kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha mchana huu UDOM
Wanafunzi Wengine wakiwa wanajaza fomu kwaajili ya kujitolea Kuchangia Damu
Wanafunzi Wa UDOM wakiwa tayari wanachuliwa damu huku wengi wakisubiri kutoa damu kwa hiari
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa tayari wameshachangia damu wakipata kinywaji mara baada ya kuchangia damu
Sehemu ambapo wanazuoni walipokua wakichukua fomu kwaajili ya kujaza na ndipo waanze zoezi zima la uchangiaji damu
Mmoja Wa Wanafunzi Salehe Mhando Akiwa anatoa damu kwa hiari
Mdau Wa Lukaza Blog Feruzi Akiwa anaandaliwa kutoa mchango wake wa damu mchana huu katika kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha.
Mwanazuoni akiwa anajaza mfuko wa kuifadhia damu
Dada akitoa damu huku akiwaeleza wenzie umuhimu wa kuchangia damu mchana wa leo katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Kijana Feruzi Akiwa katika zoezi la uchangiaji damu huku akisikilizia maumivu ya sindano ya kutolea damu
Kijana akiwa anasikilizia maumivi mara baada ya kuchomwa sindano kwaajili ya kuanza kutoa damu
..............................................
Zoezi Zima la uchangiaji wa damu katika chuo kikuu cha Dodoma kimekuja mara baada ya wanafunzi wawili wa kike ambao walikua na ujauzito kupoteza maisha wakati walipofikishwa katika hospitali ya mkoa na kuambiwa kuwa hakuna damu ya kutosha.
Zoezi Hili limekuja baada ya baadhi ya wanafunzi na viongozi kuona umuhimu wa kuchangia damu na kuzuia vifo vinavyoweza kuzuilika huku viongozi wa serikali ya wanafunzi kuingia mkataba na hospitali ya mkoa wa dodoma kuhakikisha wanafunzi atakayepelekwa hospitali hapo kutoka Chuoni na Ni Mwanafunzi apewe huduma Hiyo ya damu pale inapoonekana mwanafunzi huyo anahitaji kuongezewa damu.
oya big up BEPARI kwa hii blog, yani keep it up.What's ur secret in preparing a good blog? I once again say keep up the spirit high.by MWAKIJOLO DASTO
ReplyDeleteoya niaje bepari good work ma friend . I appreciate ur efforts just stay stronger. Man u oryaaaaaaaaaaaaa
ReplyDelete