Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Haji Mponda akisoma hotuba ya ufunguzi
rasmi wa kampeni ya Kitaifa ya kuzuiavifo vya akina mama na watoto
chini ya umri wa miaka mitano leo mchana katika viwanja vya Mnazimmoja
jijini Dar es Salaam. Dr Mponda alisema kuwa asilimia 25 ya akina mama
wajawazito wanaokufa kutokana na uzazi vifo vyao hutokana na kuvuja
damu nyingi wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua. Pia alisema
kuwa watoto wengi wanaokufa chini ya umri wa miaka mitano asilimia 22
ya vifo hivyo hutokana na kuugua ugonjwa wa malaria ambapo sababu ya
vifo ni upungufu wa damu. Dr Mponda alisema kuwa Serikali imeweka
mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa vituo vya afya na vinakuwa na
wataalamu wa kutosha. Zahanati kujengwa katika kila kijiji na Vituo vya
afya katika kila kata ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Msanii
wa mashairi Mrisho Mpoto akiwa na wanafunzi mbele ya meza ya mgeni
rasmi wakati akitoa burudani leo mchana katika viwanja vya mnazi mmoja
katika Uzinduzi wa kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto
chini ya miaka mitano
Waziri
wa afya Dr Haji Mponda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
kampeni ya kitaifa ya kupunguza vifo vya wanawake na watoto, Kushoto
ni waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto Sophia Simba.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Haji Mponda akiwa amepanda katika moja ya
piki[iki maalumu kwa ajili ya kubebea wagonjwa hususani maeneo ya
vijijini. Dr Mponda alisema kuwa serikali imejipanga kusambaza
pikipiki 421 nchini kote na tayari pikipiki 51 zimekwisha sambazwa
katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Shinyanga.
. Dr
Mponda akionesha kifurushi maalumu chenye vifaa muhimu vya
kuzalishia.Vifurushi hivyo vitaanzan kusambazwa bure kwa akina mama
wajawazito nchini kote ili kuwaepushia adha ya kununua vifaa hivyo
pindi wanapokaribia kujifungua
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Haji Mponda akipata maelekezo toka kwa
muelimishaji rika katika moja ya mabanda yaliyokuwa yakitoa huduma
katika viwanja vya mnazi mmoja leo mchana.
Moja
ya msanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo akiwa anaigiza igizo
lililokuwa na maudhui ya madhara ya uchache wa wahudum wa afya katika
vituo vya kutolea tiba hali inayopelekea akina mama wengi wajawazito
kufa kwa kukosa huduma kwa wakati. Picha zote na Mdau Victor Makinda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)