WASELA WA AMERIKA WAMEVAMIA KITUO CHA FFU WA NGOMA AFRICA BAND - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASELA WA AMERIKA WAMEVAMIA KITUO CHA FFU WA NGOMA AFRICA BAND




Ambushing in The Night !
wababe masupa staa wa Amerika wamevamia kituo cha FFU Ughaibuni
 Kianzo kimoja cha mziki cha bendi ya Ngoma Africa band,juzi kilijikuta kimevamiwa
na masupa staa wa kimerikani wapatao 350 mtandaoni, kianzo hiko cha www.myspace.com/thengomaafrica ambacho kinarusha mziki hewani kilijukuta kinapokea wageni wababe ,super stars mbali mbali kutoka Marekani ambao walishea profile ya Ngoma Africa band na kusababisha internet Sever ya myspace.com kuziwia profile ya machizi wa Ngoma Africa band aka FFU,nyenye maskani yake kule ujerumani.habari za uhakika zimetonya kuwa sababu za kuvamiwa kwa profile ya ngoma africa katika myspaceni baadhi ya nyimbo zilizomo humo,ambazo baadhi ya wadau wa mziki wa nchi za magharibi pamojana marekani wamevutiwa na mdundo huo..na kuahamua kutaka kuzitangaza kiubabe ubabe...
kwa bahati njema FFU wa Ngoma Africa band baada ya kugundua kuwa wamevamiwa..walihamishavirungu na makombora yao ya machozi(Nyimbo zao) katika Ngome yao mpya hii www.ngoma-africa.com  ambako kwa sasa wadau wote wanaweza kusikiliza. udaku utatonya kuwa FFU wamenunua Sever yaowenyewe na kuyachimbia mawe na virungu vyao vya mziki at www.ngoma-africa.com  mara nyingi tu bendi hiyo imekuwa ikikumbana mshike mshike kama kutoka kwa wadau wa mziki,kwa kile kinachoitwa "Tuwe tugawe" na FFU nao wanadai asiyefanya kazi hakuna kula!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages