WANAFUNZI WA CHUO CHA IRINGA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA VODACOM TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANAFUNZI WA CHUO CHA IRINGA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA VODACOM TANZANIA

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiwaonyesha moja ya jarida(Voda World) linalotolewa na Kampuni hiyo baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa wanaosomea kozi ya mambo ya habari walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa katika kitengo cha Mawasiliano na masoko ya kampuni hiyo hivi karibuni.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa anaesomea kozi ya mambo ya habari akiuliza swali walipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya  kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo  katika kitengo cha Mawasiliano na masoko.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa wanaosomea kozi ya mambo ya habari wakisoma jarida(Voda World) linalotolewa na Vodacom Tanzania  bure mara walipotembelea makao makuu ya kampuni ya hiyo  kwa ajili ya  kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo  katika kitengo cha Mawasiliano na masoko.

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya wa tatu kutoka kulia akiwaonyesha baadhi ya wanafunzi  wa Chuo kikuu cha Tumaini cha Iringa namna  ripoti zinavyoandaliwa na kitengo cha Mawasilino cha Vodacom Tanzania mara walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo  kwa ajili ya  kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo  katika kitengo cha Mawasiliano na masoko.
Meneja Udhamini na Matukio Rukia Mtingwa wapili toka kushoto akifafanua jambo kwa baadhi  ya wanafunzi  wa Chuo kikuu cha Tumaini cha Iringa  mara walipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania  kwa ajili ya  kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo  katika kitengo cha Mawasiliano na masoko,kushoto Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Nector Foya,kulia Meneja Mawasiliano Salum Mwalim na Ofisa rasilimali watu wa kampuni hiyo Ndihagati Biduga.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages