TIMU YA VIJANA U-23 YAIBAMIZA NIGERIA 1-0 TAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TIMU YA VIJANA U-23 YAIBAMIZA NIGERIA 1-0 TAIFA

Kocha wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 23 ya Tanzania Julio, akifurahia na kuwapongeza wachezaji wake baada ya mchezo kumalizika na timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Nigera mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Viaja U-23, wakipongezana baada ya ushindi huo.
Ebwana eeeh! Ushindi mtamu bwana asikwambie mtu, unawezafurahia na kushangilia kwa staili yeyote kwa muda huo bila kujijua, hapa mchezaji huyu akishangilia kwa staili ya aina yake ambayo kesho ukimwambia kurudia staili hiyo anaweza akashindwa kurudia kukakamaaa kama hivi.
Mchezaji wa timu ya Vijana U-23, Thomas Ulimwengu (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Nigeria, wakati wa mchezo huo.
Kocha, wachezaji na viongozi wa timu ya Nigeria wakiduwaa wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani hapo baada ya timu yao kubamizwa bao 1-0 na timu ya Taifa ya Vijana.
Mashabiki wa soka wa timu ya Taifa ya Vijana wakishangilia ushindi baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Na Sufiani 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages