Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo La Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless Lema
--
Msingi wa Maendeleo ni Haki.
“Ninawasalimu wote .
Hivi karibuni tarehe 21 Juni 2011 siku ya jumatano kuna taarifa nyingi ziliandikwa katika vyombo vya habari kuhusu muafaka dhidi ya mgogoro wa uchaguzi wa umeya uliokuwa unaendelea hapa mjini Arusha .
Ni kweli kabisa mgogoro wowote humalizwa kwa vikao na mashauriano, na ndivyo ambavyo CHADEMA tumekuwa tukitaka toka awali na mimi binafsi natamani tukae kwa amani katika nchi yenye misingi ya haki na utawala wa kuzingatia sheria. Kimsingi kabisa tulitaka serikali ya CCM itamke kuwa kosa limefanyika kwa kutozingatia kanuni ya uchaguzi wa umeya wa Arusha na kupelekea hapa tulipofika.
Mchakato wa muafaka ulipoanza mwanzoni mwa mwezi APRILI 2011 ulikuwa na nia ya kuitaka serikali ione makosa hayo na ichukue hatua kwa wahusika waliosababisha kufika katika hali tata tuliyofikia sasa na
sio kufarijiana kwa vyeo. Mgawanyo wa nafasi au vyeo ni mapendekezo tu yenye kutaka madiwani wote kushiriki utumishi kwa wananchi lakini haikuwa msingi wa madai yetu.
Baada ya kufanya utafiti na kufikiria kwa makini juu ya mchakato wa kufikia muafaka huu ndipo nilipogundua pamoja na nia nzuri ya CHADEMA, serikali ya CCM haijachukulia kwa nia na dhati ya kweli ili kutoa
majibu ya msingi ya madai yetu kuhusu HAKI na KUZINGATIA KANUNI lakini pia kuonyesha toba na ukiri wa makosa yaliyofanyika ili wananchi waweze kutuelewa.
Kwa sababu ya muafaka huu kushindwa kutoa majibu ya msingi kwa kweli siwezi kukaa kimya hata kidogo juu ya muafaka huu ambao ni udhalilishaji wa utu wa Mwanadamu na haki kwa kiwango cha hali ya juu
sana na katika mambo ya msingi tuliyokuwa tunapinga katika suala la umeya ni ukiukwaji wa haki , taratibu na sheria katika uchaguzi wa umeya uilokuwa umefanyika Arusha Mjini pamoja na sababu nyingine hii
ilikuwa ni sababu ya msingi ya kupinga jambo hili hata tukaamua kufanya maandamano tarehe 5/1/2011 yaliyopelekea watu watatu kuuwawa kikatili na polisi na wengine zaidi ya 26 kuhumizwa vibaya huku
wakiachwa na vilema vya maisha.
Hatukupinga utaratibu huo ili tugawane vyeo na nafasi mbali mbali katika manisipaa ya Arusha hili halikuwa lengo letu na kamwe haliwezi kuwa lengo langu .
Hatukuwa tunampinga Meya wa Arusha kwa dini yake au kabila lake au rangi yake tulipinga mfumo uliomchagua ambao ulikiuka utaratibu wa msingi wa kanuni na sheria za uchaguzi pamoja na mambo mengi
yaliyohusu haki na usawa ,ukweli .
Tulisema Ocd wa Arusha aondolewe na polisi washitakiwe juu ya mauwaji ya watu wasio na hatia na familia zao zilipwe fidia.
Tulitaka mkurugenzi wa manisipa ya Arusha aondolewe kazini kwa kusimamia uchaguzi batili nakusababisha majonzi mengi na vifo vya raia wasio na hatia.
Tulitaka uchaguzi wa umeya urudiwe hapa mjini Arusha na haki itendeke na sio kugawana uongozi na mambo mengi ya msingi ambayo kila mtu anajua na hata ulimwengu mzima unajua. Hivyo basi siwezi kukubali dhambi hii na udhalimu huu eti tu kwa sababu chadema imepewa unaibu meya kwani huu sio msingi mama wa
muafaka na kama suala ni unaibu Meya mbona tulimuona Diwani wa kata ya Sokoni one Mh Kivuyo kuwa ni msaliti alipokuwa ni naibu Meya ?
Ninatambua na ninajua inaweza kuwa vigumu kueleweka katika hili au kupewa tafsiri nyingi nyingi tu, napenda kujiweka wazi kuwa nitasimamia ukweli daima kwa maslahi ya wananchi na niko tayari kusimama na wananchi kukabiliana na upinzani wowote ili kuwatetea maana mimi ni mtumishi wao kwani Haki na utu sio jambo la kupuuza na kujadiliwa kwa vyeo au pesa.
Mwisho naomba mwenyezi Mungu anisaidie na watu wote wa Arusha mjini na watambue mgogoro hauwezi kuzuia maendeleo ya Arusha Mjini hata kidogo kwani hata bajeti ya 2011 -2012 ilipitishwa bila hata kuzingatia kanuni na taratibu. Kuna wafanyabiashara wachahe wa Arusha wanaoshawishiwa kuwa Haki hii tunayoitafuta inadumaza ukuaji wa biashara zao, napenda kuwaambia kuwa Mgao wa Umeme, Ufisadi, Rushwa, uonevu, kutokufutwa kwa kanuni na Ulaghai wa Serikali iliyopo madarakani ndivyo vinavyodumaza uchumi wa Taifa na Chadema inapambana ili kuhakikisha inajengwa Tanzania Mpya yenye kufuata Kanuni na
utaratibu na mfumo wa sheria utakaoleta Neema ya kweli Tanzania.
Ni nayo ilani yangu kwa wananchi wa Arusha nitatimizakwa mipango yangu na yale ya kisera yanayohusu Nchi nitaendelea kuongea kwa nguvu zote kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutumia vyombo vingine kama Mbunge.
Na pia niwaombe Madiwani Wafikirie kwa makini utashi wenu dhidi ya jambo hili nimatumaini yangu mtakuwa mlifanya maamuzi kwa haraka sana bila kiuzingatia ukweli.
Arusha nawaomba sana na mnapaswa kuwa wavumilivu na majasiri wakati huu ambapo tunapita katika majaribu mengi katika kupigania ukweli ,hatuwezi kuudhalisha utu wa mwanadamu na haki kwa kugawana
vyeo kwa kisingizio cha maendeleo, Hata hivyo hakuna maendeleo Duniani yanayopita haki ,ukweli , utu , usawa ,na kama kuna mtu yeyote anafikiri anaipenda Nchi yake basi awe mfano wa kufikiria na kutenda
Haki .
Msiogope Mungu yuko pamoja nasi Ukweli utashinda. Mungu Awabariki
sana.
GODBLESS J LEMA ( Mbunge Arusha Mjini )-CHADEMA
…………………..........
27/6/2011.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)