Kocha
wa timu ya Taifa Stars Jan Paulsen na Meneja wa Mahusiano na Jamii wa
kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela wakipanda mti kwa pamoja
wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira, zoezi hilo limefanyika
katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo leo,
anayeshuhudia tukio hilo katikati ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Magesa
Mulongo.
Golikipa
wa timu ya taifa Taifa Stars Shaban Kado akipanda mti katika viwanja
vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, wakati kampuni ya bia ya
Serengeti ilipoadhimisha wiki ya mazingira kwa kupanda miti 400 katika
wilaya ya Bagamoyo kama ishara ya kampuni hiyo kuthamini na kutunza
mazingira, Kilele cha maadhimisho hayo duniani kote kitafanyika Juni 5,
mwaka huu.
Wafanyakazi hao leo wakishirikiana na timu ya Taifa Stars na wananchi
wa Bagamoyo wamepanda miti 400, huku lengo likiwa ni kupanda miti elfu
20.000 mpaka Juni 5 ambayo ndiyo siku ya kilele cha wiki ya mazingira
katika mikoa ya Pwani, Kilimanjaro na Mwanza, ikiwa ni kuhakikisha
mazingira yanaboreshwa na kutunzwa vyema huku wakitoa wito kwa jamii
kutunza miti hiyo ili iweze kukua vizuri na kuboresha mazingira yetu.
Waliosimama katika picha kutoka kulia ni Henry Joseph mchezaji wa timu
ya Taifa, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Magesa Mulongo, kocha wa timu ya
Taifa Stars Jan Paulsen na kushoto mwenye kofia ni meneja Mahusiano na
Jamii wa Serengeti Nandi Mwiyombela pamoja na wachezaji wa timu ya
taifa.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Magesa Mulongo akipanda mti katika viwanja vya
ofisi yake wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira ambapo
wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti pamoja na wachezaji wa timu
ya Taifa wameshiriki katika zoezi hilo lililofanyika leo mjini Bagamoyo
wanaoshuhudia tukio hilo ni Kocha wa Taifa Stars, wachezaji pamoja na
wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)