Wanafunzi Wa Udom Wakiwa wamekusanyika jioni hii mbele ya bweni namba tatu na kwenye uwanja wa mpira wa kikapu kwaajili ya kukutana na Waziri wa Elimu Mh Shukuru Kawambwa Huku wakiwa wametoa Angalizo Kwa Waziri Kawambwa wakati wanafanya kikao na uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi kabla hajaja basi maraisi wa vitivyo viwili pamoja na wanafunzi walioshikiliwa na polisi waachiwe la sivyo watawafuata huko huko na waziri hatofika kabisa
Wanafunzi Wakiwa Kwenye Makundi wakijadili Ni jinsi gani Uongozi Pamoja Na Waziri Kawambwa wanaweza kuendesha Kikao na Uongozi wa Chuo wakati raisi wa kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha na wa kitivo cha sayansi asilia pamoja na wanafunzi wengine wmeshikiliwa na polisi.
Wakisikiliza Wakati uongozi wa wanafunzi ukiongea na simu na mmoja wa viongozi wa wanafunzi kuwa wasiendelee na vikao kama maraisi pamoja na wanafunzi wengine hawajaachiwa huru wakishindwa kufanya hivyo basi wanafunzi watavamia jengo la ofis kwa kushinikiza waziri wa elimu atoe amri waachiwe
Taarifa zilizopata mtandao huu muda huu ni kuwa maraisi wote wawili pamoja na wanafunzi wameachiwa huru muda huu na wanafunzi wanaelekea kuwapokea wanafunzi wenzao pamoja na maraisi wao getini
Vuta subira matukio Zaidi Yanakuja
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)