Mgambo
wakivunja baadhi ya maboksi ambayo hutumiwa na watengeneza saa na
wachonga mihuri katika makutano ya mitaa ya Msimbazi na Uhuru leo
jijini.
WAFANYABIASHARA ndogondogo katika soko la Kariakoo, jijini Dar es
Salaam, bado wanakumbana na adha kutokana askari wa jiji kuwachukulia
vitu vyao kwa nguvu na kutoweka navyo.
Wakizungumza leo na kamera yetu, wafanyabiashara hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa hali si shwari kwao kutokana na kuburuzwa mara kwa mara na mgambo wa jiji.
Wakizungumza leo na kamera yetu, wafanyabiashara hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa hali si shwari kwao kutokana na kuburuzwa mara kwa mara na mgambo wa jiji.
Gari la kuzolea taka likiwa limezungukwa
na uchafu jirani na soko la Kariakoo. Wafanyabiashara wamedai kuwa
mlundikano huo wa uchafu unatoa harufu kali inayowafanya kufanya
shughuli zao kwa taabu pia kuhatarisha afya zao, hivyo wameiomba
Halmashauri ya Manispaa Ilala kushughulikia kero hiyo haraka.
Mama wa Kimaasai ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja
akiondoka eneo la kuuzia biashara zake baada ya askari wa jiji kusomba
meza yake ya biashara na bidhaa zake za asili eneo la Kariakoo, leo.
PICHA/HABARI NA HARUNI SANCHAWA /GPL.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)