Mkurugenzi
wa Radio One Stereo Deogratius Rweyunga akitoa shukrani kwa kampuni ya
MeTL kwa kuona umuhimu wa kuchangia ili kufanikisha mashindano hayo na
kuzitaka kampuni zingine kuiga mfano huo.
Afisa
Uhusiano wa MeTL Esther Dotto akielezea jinsi Mheshimiwa Mbunge wa
Singida Mjini alivyoguswa na Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo
na kuahidi kuendelea kushiriki zaidi katika kuhakikisha Tanzania
inafanikiwa kimichezo.
Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya MeTL ambaye pia ni msaidizi wa Mh. Mohammed
Dewji (Mb) Esther Dotto akikabidhi mchango katoni 42 za maji safi ya
kunywa ‘ MAISHA’ yanayotengenezwa na Kampuni ya A-ONE Products and
Bottlers ambayo ni moja ya makampuni ya MeTL kwa Mkurugenzi wa Radio
One Deogratius Rweyunga kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya riadha
ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 3-4 June, 2011.
Mh. Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini.“Ni
vyema sisi kama watanzania tukachangia kukuza maendeleo yetu wenyewe
katika michezo, na si katika soka peke yake, bali kwa michezo yote kwa
ujumla”
Katoni
za maji safi ya kunywa aina ya MAISHA yanayotengenezwa na moja ya
kampuni ya MeTL yaliyokabidhiwa kama mchango kwa ajili ya mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)