Baadhi ya waliokuwa washiriki wa shindano la Miss Utalii lililopita wakifuatilia kikao cha tathiminI.
Katikati
ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA),Bi.Vivian Shalua akisisitiza jambo wakati wa tathimini ya
shindano la urembo la utalii iliyofanyika wiki hii kwenye Ukumbi wa
Baraza hilo.Kulia kwake ni Muandaaji wa shindano hilo Bw.Gideon
Chipungahelo na Mratibu Rajab Zubwa.
Afisa
Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Idara ya Utamaduni
Bw.Michael Kagondela akitoa michango ya uboreshaji wa shindano la Miss
Utalii kwenye kikao cha tathimini kilichofanyika wiki hii Ukumbi wa
BASATA.
Rais
wa Miss Utalii ambaye pia ni muandaaji wa Shindano la urembo la
utalii,Bw.Chipungahelo akitoa maelezo kuhusu shindano lake kwenye kikao
hicho cha tathimini.Kushoto kwake ni Bi.Shalua.
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha kikao maalum cha kutathimini
shindano la urembo la utalii (miss utalii) linalofanyika kila mwaka
ambapo wito umetolewa kwa waandaaji wa shindano hilo kufuata kanuni na
taratibu zilizopo.
Akizungumza
kwenye kikao hicho kilichofanyika wiki hii kwenye Ukumbi wa
BASATA,Mkurugenzi wa Idara ya ukuzaji Sanaa wa baraza hilo,Bi Vivian
Shalua alisema kwamba,shindano la miss utalii limebeba utambulisho wa
taifa hivyo waandaaji hawana budi kujipanga na kufanyia kazi mapungufu
yote yanayokuwa yanajitokeza
“Kumekuwa
na mapungufu mengi katika mfumo mzima wa uendeshaji wa shindano
hili,kamati haionekani, mambo mengi yamekuwa yakifanyika kinyume cha
makubaliano na maandishi yaliyopo.Hata mratibu wa shindano kutoka
BASATA amekuwa hahusishwi katika masuala kadhaa” alisema Bi.Shalua
wakati akitaja baadhi ya mapungufu yanayopaswa kufanyiwa kazi haraka.
Aliongeza
kwamba,katika kutangaza vivutio vya utalii shindano hilo limekuwa
likijikita katika maeneo ambayo tayari yanafahamika na ya eneo moja tu
badala ya kwenda katika vivutio mbalimbali vilivyo katika kanda tofauti
hapa nchini na kutumia mavazi na ngoma kutoka makabila mbalimbali.
Awali
wakitoa michango yao, pamoja na kupongeza wazo na uwepo wa shindano
lenyewe, wajumbe kutoka kada mbalimbali ndani ya jamii walishauri
kuangaliwa upya kwa mfumo wa uendeshaji wa shindano hilo ambapo walitaka majukumu ya kamati ya uendeshaji shindano hilo yawekwe wazi.
Aidha,walitaka
maandalizi ya mapema ya shindano ikiwa ni pamoja na kutimiza kanuni na
taratibu mbalimbali za kulifanya lifane na kuvutia watu wengi zaidi
tofauti na lilivyo sasa ambapo limedunishwa kutokana na mfumo wake wa
uendeshaji.
“Shindano
la Miss Utalii ni kubwa sana kuliko yote,ndilo limebeba nembo ya
kitaifa ni lazima kwanza litangazwe na lifahamike pia washiriki
wasiandaliwe kwa ajili ya kuwakilisha shindano tu bali pia
kuliwakilisha taifa” alisema Michael Kagondela ambaye ni Afisa Kutoka
Wizara ya Habari,Vijana,utamaduni na Michezo idara ya Utamaduni.
Aliongeza
kwamba,kumekuwa na dhana mgando miongoni mwa waandaaji wa mashindano ya
urembo nchini ya kuwaandaa washiriki katika kuyawakilisha mashindano
yao badala ya taifa zima hali ambayo imekuwa ikisababisha wafanye
vibaya kutokana na kukosa uungwaji mkono miongoni mwa watanzania walio
wengi.
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) liko kwenye mchakato wa kuyapitia na kuyapa
taswira mpya mashindano ya urembo nchini ili yawe na mfumo wa uwazi
katika uendeshaji na zaidi kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizopo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)