Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Bwana Aaron Williams, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la huduma za kujitolea za Wamarekani (American Peace Corps)ikulu jijini
Dar es Salaam leo asubuhi wakati mkurugenzi huyo na ujumbe
walipomtembelea na baadaye kufanya mazungumzo.
Rais
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso
Lenhardt, wakiweka saini katika ramani ya duania inayoonyesha sehemu
mbali mbali duniani ambapo Shirika la huduma za kujitolea za
Wamarekani(American Peace Corps volunteer) linatoa huduma ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu shirika hili lilipoanzishwa.Wengine katika picha aliyesimama kushoto ni Mkurugenzi
mkuu wa Shirika hilo duniani, Bwana Aaron Wiliams, na kulia,a liyesimama
ni Mkurugenzi wa shikika hilo nchini Bi.Andrea Wojnar Diagne. Shirika
la Peace Corps lilianzishwa mnamo Tarehe moja Machi mwaka 1961 na
aliyekuwa Rais wa Marekani hayati John F.Kennedy. Hapa nchini jumla ya
wanachama 2100 wa shirika hilo walitoa huduma mbalimbali kuanzia mwaka
1961 katika sekta za Elimu, Utunzaji waMazingira na afya. Kwasasa jumla
ya wanachama 140 wa shirika hilo wanafanya kazi za kujitolea katika
sehemu mbalimbali nchini wakifundisha masomo ya Sayansi,Hesabu na lugha
ya kiingereza.
Picha na Freddy Maro
Source: John Bukuku - Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)