William Ngeleja waziri wa Nishati na Madini
---
Na Nova Kambota
Kama kuna jambo
linalowaumiza vichwa watanznia basi ni swali kuwa kwanini kila
wanalopanga halifanikiwi? au kwanini wananchi ni masikini licha ya
maliasili zilizojaa kila kona yanchi hii? Wakiangalia elimu hoi watoto
wanafeli, wakija kwenye afya hakuna kitu, wakienda kwenye kilimo na
hata umeme tabu tu kwa kifupi hakuna jipya ni uduni na ubabaishaji
mtupu.
Katika lindi la mawazo ya namna hii au maswali mengi yasiyojibika tunawatazama viongozi wetu na uwajibikaji wao usiokidhi viwango kiasi kwamba wamepwaya mno , wajuzi wa kuzungumza bila kutenda, ni watu wa blah blah na porojo tu.
Kwakweli Tanzania imetawaliwa na wapiga porojo hebu angalia kwenye hiyo kaulimbiu ya “kilimo kwanza”inavyotangazwa na kupigiwa chapuo na viongozi wetu kasha nenda huko vijijini kwenye mashamba utaona hata mabwana shamba hakuna na hizo pembejeo zenyewe za kilimo hakuna, sasa utasema hapo kuna kilimo kwanza au porojo tu?
Serikali nayo
imeshindwa kuweka huduma za nishati ya umeme wa uhakika, sasa naona ina
mchoko naam! Huu ni mchoko ndio maana kila kwenye hotuba tunapigwa
kalenda mpaka mwaka huu au ule tatizo la umeme litakuwa historia halafu
mda huohuo umeme ni wa mgao, waziri wa nishati nay eye hana jipya bado
watu tunateseka kwa sababu ya kukosa ubunifu na uzalendo , mwenyekiti
wa kamati ya bunge ya nishati anataka tuwashe mitambo ya Dowans, watu
wanahoji anataka turudi tulipotoka? Hizi kama sio porojo nini basi?
Nchi ipo gizani viongozi wanapiga porojo inasikitisha sana.
Tabia ya kupiga porojo inaendelea kudidimiza nchi , hata kwenye michezo tunapiga porojo halafu tunataka kucheza kombe la Dunia,bungeni kuna porojo kiasi kwamba bunge linafanywa sehemu ya kupigana vijembe na mipasho halafu na sisi tunaamini iko siku tutakuwa kama wenzetu wa Ulaya na Marekani ambao tayari wamefuta blah blah na porojo kwenye kamusi za vichwa vyao wanafanya mambo kizalendo na kwa kujituma, haiwezekani !
Matokeo ya porojo yanapoonekana viongozi wetu hawachelewi kusikitika na kuhidi kujirekebisha, ona matokeo ya kidato cha nne yalivyowaumbua viongozi sasa wanajifanya wamejifunza hakuna kitu porojo tu , mabasi yanakimbia yanavyotaka wenye jukumu la kulinda usalama barabarani wanapiga porojo watu wanakufa utadhani ni msimu wa ajali.
Siku hizi hadi viongozi wa dini wamekumbwa na tabia ya kupiga porojo , badala ya kutetea wanyonge wao wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kujigeuza miungu watu wanadanganya masikini na kuwakamua hata kidogo walichonacho na wengine wamejigeuza watabiri wanatabiria watu kufa? Hizi ni porojo tupu.
Sasa katika muktadha huu ndio maana najiuliza kuwa nchi hii iliyolewa kwa wingi wa porojo itaendelea vipi? Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma kwasababu ya porojo zisizokwisha na hazina mipaka hata kwenye mambo ya msingi tunapiga porojo au ndio tunategemea kuendelea kwa miujiza ya Mussa? Tafakari!
Nova Kambota Mwanaharakati,
0717 709618 au +255717 709618
Tanzania, East
Africa,
June
30, 2011
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)