MAKAMU WA RAISI DK BILAL ALIPONGURUMA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAISI DK BILAL ALIPONGURUMA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini New York.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake, mbele ya viongozi waalikwa katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon, wakati alipokutana naye kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New York, jana Juni 8, 2011 baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, akisalimiana na Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakati waziri huyo alipoongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) New York kwa ajili ya mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ( wa tatu kushoto) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon (wa tatu kulia) kwa ajili ya mazungumzo jijini New York.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages