MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA DK ASHA-ROSE MIGIRO, NEW YORK - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA DK ASHA-ROSE MIGIRO, NEW YORK

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea hotelini alikofikia jijini New York, jana Juni 10, 2011 na kufanya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea hotelini kwake jijini  New York,  jana Juni 10, 2011 na kufanya naye mazungumzo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea jana Juni 10, 2011 na kufanya naye mazungumzo.
Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Dkt. Mohammed Bilal, Akiwa Katika Mazungumzo Na Naibu Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, Wakati Katibu Huyo Alipomtembelea Na Kufanya Naye Mazungumzo
Naibu Katibu Mkuu UN, Dkt. Asha Rose Migiro, Akimkabidhi Zawadi, Makamu Wa Rais, Dkt. Mohammed Bilal
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha rose Migiro, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Hoteli Intercontinental, alipofikia Makamu New York, jana Juni 10, 2011. Wa pili kushoto ni mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kulia), mkewe Mama Zakhia Bilal (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro (wa nne kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim (wa pili kulia) na mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lediana Mng’ong’o (kulia). Kutoka (kushoto) ni Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, Naibu Waziri wa Afya ,  Sawere Nkya, Waziri wa Afya wa SMZ, Juma Duni Haji na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais SMZ, Fatma Fereji, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo baina ya Makamu wa Rais na Naibu Katibu Mkuu jana Juni 10, 2011, New York.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York jana Juni 10, 2011, kwa ajili ya kuhudhuria hatua ya ufungaji wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi, uliozishirikisha nchi zaidi ya 30. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages