Katibu
Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Phillemon Luhanjo akitoa
ujumbe wa wiki ya Utumishi wa Umma kwa waandishi wa habari (hawako
pichani) ambapo amesema matumizi ya mipango mkakati, mikataba ya kazi,
mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, upimaji wa wazi wa utendaji kazi na
mfumo wa kushughulikia malalamiko ni mambo ambayo yatatiliwa mkazo
katika utumishi wa Umma.
Bw.
Luhanjo akielezea matarijio ya Utumishi wa Umma kwa siku zijazo ambapo
amesema ni kuendelea kuelimisha na kuwakumbusha watumishi wa Umma
umuhimu wa kubadilika kifikra ili Utumishi wa sasa na baadaye uwe ni
utumishi wezeshi na unaowajibika ipasavyo.Picha na Geofrey Mwakibete
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)