Mkurugenzi
wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza wakati
wa uzinduzi rasmi wa usamabazaji wa bia za Serengeti Lager,
zinazozalishwa na kiwanda hicho kipya katika mji wa Moshi mkoani
Kilimanjaro na vitongoji vyake ikiwemo na mikoa ya jirani ,uliofanyika
jioni ya Jana ambapo uzinduzi huo uliambatana na msafara mkubwa wa
magari uliozunguka katikati ya mji wa moshi huku msafara huo ukiongozwa
Mkurugenzi huyo, Richard Wells,sambamba na wafanyakazi wa kampuni
hiyo,shamra shamra hizo zilinogeshwa zaidi wakati wafanyakazi wa kampuni
hiyo walipoamua kugawa bure kinywaji hicho cha Serengeti katika maeneo
mbalimbali.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza mbele ya
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwemo
wafanyakazi wa kiwanda hicho,wakati wa uzinduzi rasmi wa usambazaji wa
kinywaji hicho,uliofanyika jioni ya jana,kulia kwa Mkurugenzi ni Mkuu wa
Mahusiano na jamii- Moshi Bwana Mandala akisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells wakiteta jambo na
Mkuu wa Mahusiano na jamii (Moshi), Bwana Mandala.
Pichani
kati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells
akisalimiana na mdau mkubwa wa kinywaji cha Serengeti Lager,Loui
Kifwanga aliyefika pia kushuhudia uzinduzi rasmi uliofanyika jioni ya
jana kiwandani hapo,na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na jamii (Moshi),
Bwana Mandala
Pichani
kati alienyoosha mkono juu ni Mkurugenzi wa kampuni ya Serengeti
Breweries (SBL),Richard Wells akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa
idara ya usambazaji kabla ya kuondoka kiwandani hapo jioni ya jana
Pichani
kulia ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager,Allan Chonjo
wakifurahia na mdau wa mwingine wa kampuni hiyo kuzinduliwa rasmi kwa
kiwanda hicho katika mchakato mzima wa kusambaza kinywaji chake.
Meneja
wa Kinywaji cha Serengeti Lager,Allan Chonjo pamoja na wafanyakazi
wenzake wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi kufanyika jioni ya
jana kiwandani hapo,mjini Moshi.
Gari
ikitoka kiwandani hapo ikiwa tayari imesheheni mzigo tayari kwa
kuwapelekea wateja,huku wafanyakazi wa kampuni hiyo wakitia baraka zao
kwa kupiga makofi kwa pamoja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti wakiwa bize jioni ya jana mara baada ya uzinduzi rasmi.
Mlima Kilimanjaro uonekanavyo kwa nje ya kiwanda hicho.
Mmoja
wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akipakia bia katika gari kwa kutumia
mashine maalum ya kunyanyulia mizigo kiwandani hapo,tayari kwa
kuwasambazia wateja wao popote pale.
Pichani
ni msafara wa magari ukikatiza katikati ya mji wa Moshi jioni ya jana
kuashiria kuwa tayari bia aina ya Serengeti imeanza rasmi kuzalishwa
ndani ya mji huo kwa wateja wao.Magari hayo yalikuwa yamepambwa kwa
maandishi makubwa 'Kiwanda chetu,Bia Yetu !
Huu
ndiyo muonekano wa kiwanda cha Kampuni ya bia ya Serengeti mjini Moshi
katika mkoa wa Kilimanjaro kilichozindua rasmi usambazaji wa bia zake
mara baada ya kuanza uzalishaji jioni ya jana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)