KIKOSI CHA U23 CHATUA SALAMA LAGOS KULINDA HESHIMA LEO JIONI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIKOSI CHA U23 CHATUA SALAMA LAGOS KULINDA HESHIMA LEO JIONI



Na Boniface Wambura, Lagos
Timu ya U23 imewasili salama hapa saa 6.30 mchana kwa ndege ya Kenya Airways kabla ya kuunganisha ndege ya Concord Airlines kwenda Benin City ambapo mechi dhidi ya Nigeria itachezwa kesho kuanzia saa 10 kamili saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 12 kamili jioni.
Awali U23 ilikuwa ifike nchini humo saa 4 kamili asubuhi, lakini ikachelewa kutoka Nairobi ambapo ilitoka saa 3.30 badala ya saa 1.30 baada ya ndege ya Kenya Airways kuchelewa kuondoka.
Kocha Jamhuri Kihwelo amesema vijana wake katika hali nzuri ya kupeperusha
bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambapo mshindi baada ya matokeo ya
nyumbani ambapo U23 ilipata ushindi wa bao moja ataingia katika hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini
London, Uingereza.

Amesema timu yake itacheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza huku akijaza viungo wengi kwa lengo la kumiliki mpira kwa muda mrefu, hivyo kuzuia
mashambulizi ya timu pinzani kwa staili.
Kihwelo amesema mbele atatumia washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata.
Wachezaji wengine aliokuja nao hapa ni Jamal Mnyate, Jackson Wandwi, Hussein
Javu, Mohamed Soud, Obadia Mungusa, Abuu Ubwa, Juma Abdul, Abdul Juma, Himid Mao, Issa Rashid, Khamis Mcha, Salum Abubakar, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Godfrey Wambura na Awadh Juma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages