" Kambona , ah, ah!
Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"
Utotoni nilipata kuwasikia kaka zetu wakiimba wimbo
huo wa mchakamchaka. Nikiwa shuleni nimesoma sana habari za siasa za wakati huo.
Bado naendelea kusoma na kujifunza. Katika kusoma kwangu nimeona, kuwa suala la
ugomvi wa Oscar Kambona na Julius Nyerere alikuwa rahisi vile kama tulivyoambiwa
na hata kuimbiwa. Simulizi za Oscar Kambona zinabaki kwa wengi kuwa ni za upande
mmoja.
Hakika, si wengi wenye
kufahamu nini hasa kiliwatokea marafiki watatu hawa; Julius Nyerere, Oscar
Kambona na Rashid Kawawa. Kizazi hiki cha sasa cha Watanzania kinaweza kunufaika
sana na uelewa wa yaliyojiri katika harakati za kisiasa za wakati huo
zilizopelekea uhuru wa Tanganyika na baadae Oscar ' Kujivua' gamba kwa
kutokubaliana na rafiki yake Julius juu ya Azimio la Arusha. Kuna maswali ya
kujiuliza; Je, ugomvi wa Oscar na Julius ulianzia kwenye Azimio au kabla ya
hapo? Je, umma ulipotoshwa juu ya nini kilichotokea? Ikumbukwe, Oscar na Julius
walikuwa marafiki wa kushibana kiasi cha Julius kuwa ' Mpambe' wa Oscar kwenye
ndoa yake iliyofanyika London. Je, Rashid alichangia kwenye ' kutoswa' au '
kujitosa' kwa Oscar. Kwamba Oscar aliona hakupata kuungwa mkono na Rashid. Je,
Oscar alifanya makosa kwa kuondoka nchini badala ya kubaki na kupambana kwa hoja
na rafiki yake Julius?
Je, nianze kuwasimulia machache niliyojitahidsi kuyajua, au niwaache kwanza wengine msimulie mnayoyajua, maana, kuna wanaodhani wanajua na kuna wanaojitahidi kujua. Mie niko kwenye kundi hilo la pili!
Na
Maggid
Mjengwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)