Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Wakimsikiliza Kwa Makini Waziri Mkuu Wa Kitivo Muhumuzi William
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini waziri mkuu wa kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Mh William Muhumuzi Juu ya maamuzi yaliyofikiwa na uongozi wa chuo na Uongozi wa wanafunzi katika kikao chao na waziri wa elimu
Wanafunzi Wakijadili juu ya hali iliyopo chuoni hapa kwa sasa mchana huu
Wanafunzi Wakitawanyika Mara baada ya Kutoa na kufikia maamuzi Ya Kuendelea na mgomo hap kesho
Mwanafunzi Mmoja Adumbukia Kwenye Mtalo Wakati wakitawanyika
Wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya jamii sanaa na lugha wamekutana mchana huu na kufikia maamuzi ya pamoja na kuamua kuendelea na mgomo wao ulioanza alhamisi iliyopita kwa madai ya kwamba serikali imezidi siasa na kushindwa kutekeleza maswala yao
Wakati huo Wanafunzi Hao Wameamua kuendelea na Mgomo Huo mara baada ya barua kutoka kwa waziri ya elimu Shukuru Kawambwa kusomwa na Wanafunzi hao kuichanganua kiunaga ubaga Na Kuikataa barua hiyo Kwa sababu ya kwamba mwanzo alifika chuoni na alihahidi lakini tokea ahadi ni miezi saba sasa je itawezekanaje ndani ya wiki mbili waweze kutatua tatizo hilohilo waliloshindwa kutatua ndani ya miezi saba aliyoahidi waziri wa elimu Shukuru Kawambwa. Kwa hiyo wanafunzi hao wameendelea na Mgomo ambapo sasa ikifika kesho inakuwa ni siku ya tatu na hatihati chuo kufungwa sababu ya mgomo kuchukua siku tatu mfululizo
Muda si Mfupi taarifa zilizotufikia hapa Ni Kwamba Wanafunzi Wote wa Mwaka Wa Pili Wanaosoma Shahada Ya Kwanza Ya Mahusiano ya Kimataifa Na Watu Zaidi Ya Sitini Kuondoka Chuoni Hapa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)