JUST IN: KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII SANAA NA LUGHA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUTOKANA NA MGOMO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JUST IN: KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII SANAA NA LUGHA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUTOKANA NA MGOMO

 Mida ya asubuhi ya leo wanafunzi walipokutana tena mbele ya bweni namba tatu kwaajili ya kuhakikisha wanafunzi waliosimamishwa masomo wanarudishwa
 Wanafunzi wakijadiliana na hatimaye walipokubaliana kwenda kwenye ofisi ya Mkuu Wa Kitivo kwaajili ya kushinikiza wenzao waliosimamishwa masomo warudishwe au wasiporudishwa basi waondoke wote kwenda nyumbani
 Wanafunzi Wakikinga Maji kwaajili ya kujizuia na mabomu ya machozi endapo yatapigwa na askari wa kutuliza ghasia asubuhi ya leo mara baada ya kuwaona askari wa kutuliza ghasia wakilandalanda maeneo ya chuoni hapo
 Umati wa wanafunzi ukiwa umekusanyika mbele ya ofisi ya mkuu wa kitivo asubuhi ya leo
 Wanafunzi wakiwa wanarudi mabwenini kwao kwaajili ya kuchukua vilivyo vyao mara baada ya mkuu wa kitivo kukifunga chuo hiko kwa muda usiojulikana


 Mara baada ya kupewa masaa sita kutoonekana maeneo ya chuo wanafunzi wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari ya kuelekea makwao asubuhi ya leo ndani ya chuo kikuu cha dodoma
 Makamu wa Raisi wa kitivo cha sayansi ya jamii sanaa na lugha Mh Swai akiwasiliana na Mwenye teksi kwaajili ya kumfuata chuo mara baada ya chuo kufungwa kwa muda usiojulikana
 Hapo ni maeneo ya mjini standi kuu ya mkoa wa dodoma wanafunzi wakisubiri mabasi huku wengine wakiwa wamekosa magari ya kwenda makwao kwa siku ya leo
 Wakisubiri Mabasi wakati wakiwa standi ya mkoa wa dodoma kwaajili ya safari za kuelekea makwao
Hali ilivyokua asubuhi ya leo maeneo ya jamatini standi ya mkoa wa Dodoma leo asubuhi

Hatimaye Kitivo cha sayansi ya jamii sanaa na lugha cha chuo kikuu cha dodoma kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo ulidumu kwa siku tatu.

Mgomo huo ulikua ni kwaajili ya kudai mafunzo kwa vitendo ambapo awali waziri wa elimu Shukuru Kawambwa aliwaahidi wanafunzi hao kwamba ndani ya wiki mbili tokea tarehe 23 disemba 2010 wanafunzi wote wasio na mafunzo kwa vitendo wataenda lakini wiki iliyopita tume ya vyuo vikuu Tanzania walitoa tangazo kwamba hakuna kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kozi zilizokua hazina mafunzo kwa vitendo mpaka chuo kitakapotoa prospectus mpya

Chuo Kimefungwa Kwa Muda usiojulikana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages