Baada ya Waziri Wa Elimu Na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mh Shukuru Kawambwa Kuahidi kuja kuongea na wanafunzi kwa mara nyingine tena mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa chuo kushindwa kufika kuongea na wanafunzi kwasababu ya kikao kuchukua muda mrefu hapo jana.
Wanafunzi wameendelea na mgomo huo kwa kutokuingia darasani hadi pale atakapokuja kuongea na kueleza ni lini pesa za mafunzo ya vitendo zitaingizwa na je wataenda kufanya mafunzo kwa vitendo, wanafunzi hao wametoa masharti kwa waziri huyo mwenye dhamana ya elimu nchini kwa kuwatuma viongozi wao wamwambie Waziri Kawambwa kuwa hawatakia siasa kama alivyowaahidi tarehe 23 disemba 2010 na akija aje na majibu ya kuwa kabla ya kufanya mitihani ya mwishoinayotarajiwa kuanza tarehe 20 june 2011 jumatatu ijayo pesa iwe imeshaingia na msimamo waliotoa wanafunzi ni kuwa hawataingia darasani mpaka pesa ya field (mafunzo kwa vitendo) itakapoingia.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)