IFM MABINGWA WA SAFARI LAGER POOL HIGHER LEARNING - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

IFM MABINGWA WA SAFARI LAGER POOL HIGHER LEARNING

Wanafunzi wa timu ya Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakishangilia na Kombe mara baada ya kuibuka washindi wakati wa fainali mashindano ya Safari Lager Pool Higher Lerning yaliyomalizika jana mijini Dodoma mashindano hayo yalifanyika katika ukumbi wa polisi jamii uliopo mjini dodoma
Nahodha wa timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Rashid Mashaka (kulia) akiwaonyesha wenzake kitita cha Shilingi milioni mbili na nusu mara baada ya kukabidhiwa ikiwa ni mabingwa wa mashindano ya fainali za Safari Lager Pool Higher Lerning yaliyomalizika jana mjini Dodoma

Na Michael Machellah –Dodoma

CHUO cha usimamizi wa Fedha (IFM) kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Pool Higher Lerning yaliyomalizika jana mjini Dodoma kwa kuwachapa chuo cha St. Agustini (SAUTI) cha mwanza 13-6.


Dalili za IFM kutwaa ubingwa zilionekana tangu mwanzo wa mashindano ya fainali hizo kwani walifungua mashindano hayo na Chuo hicho cha SAUTI ambacho wamekuja kukutana tena fainli kwa kuwafunga 13-10,baadae wakakutana na chuo cha SUA cha Morogoro wakashinda 13-3 na pia wakakutana na Chuo cha Tumaini Moshi wakashinda 13-2 wakawa tayari wameshafanikiwa kutinga nusu fainali nakukutana na wenyeji wa mashindano ambao ni chuo cha St. John ambapo pia swalibuka na ushindi wa 13-4. na kufanikiwa kuingia fainali na ndipo walipokutana tena na timu ya chuo cha SAUTI Mwanza na kuitwanga 13-4


IFM katika ushindi huo walizawadiwa Shilingi milioni mbili na nusu pamoja na Kombe ambapo washindi wa pili ni SAUTI mwanza walijitwalia zawadi ya Shilingi Milioni moja na nusu na washindi wa tatu ni wenyeji Dodoma kutoka chuo cha St.John ambao walijitwalia zawadi ya Shilingi Milioni moja na laki tatu na washindi wa nne ni Chuo cha Tumaini Moshi ambacho kilipata zawadi ya Shilingi milioni moja na timu zote zilizoshiliki zilipewa kifuta jasho cha shilingi laki tano kila moja.


Upande wa wachezaji mmoja mmoja fainali waliingia Charles Venance kutoka IFM Dar es Salaam na Obiara Anyoti kutoka St. John Dodoma ambapo Mtoto wa Mjini Posta Jijini Dar es Salaam,Charles Venance (Mesi) alionyesha maajabu kwa kumchapa mpinzani wake Obiara 4-2 hivyo kutwaa ubingwa upanda wa Singles na kuzawadiwa kitita cha Shilingi laki tatu na mshindi wa pili Obiara Anyoti kibuka na shilingi laki mbili na mshindi wa tatu Emanuel alipata shilingi laki moja na elfu hamsini


Timu shiliki katika mashindano hayo zilikuwa n inane kutoka katika mikoa minane ambazo na IFM Mabingwa kutoka Dar es Salaam, SUA morogoro, Ruaha Iringa, St.John wenyeji wa mashindano Dodoma,SAUTI Mwanza,Tumaini Moshi,Mist Mbeya na TAA cha Arusha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages