BENKI YA KCB TANZANIA TAWI LA MOROGORO LAPANDA MITI YALIONI 3.5 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA KCB TANZANIA TAWI LA MOROGORO LAPANDA MITI YALIONI 3.5


Mjumbe wa Kamati ya shule ya Msingi Msamvu B, Nassoro Korwe akisisitiza jambo mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti 600 iliyotolewa na Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro. Kushoto ni Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis na kulia ni Meneja Muendeshaji wa benki hiyo Hogla Laiser.
Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Carlos Msigwa akimkabidhi mti Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis wakati wa zoezi la upandati miti 600 kwa shule ya msingi Msamvu B kati ya 21,000 iliyotolewa na benki  ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Afisa Biashara wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Leila Kisinda na mfanyakazi mwenzake wakiteta jambo wakati wa zoezi la upandaji miti 600 kwenye Shule ya Msingi Msamvu B Morogoro lililowashirikisha walimu na wanafunzi wa shule hiyo  ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti 21,000 iliyozinduliwa hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msamvu B, Edidadi Ikomba (Katikati) akimuonesha mfanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania eneo la shule hiyo  litakalopandwa miti 600 kati ya 21,000 kwa ajili ya kampeni iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam. Kulia ni baadhi ya wanafunzi wakimwagilia miti iliyopandwa.
Kashinde Juma ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya shule ya msingi Msamvu B iliyopo mkoani Morogoro akimwagilia maji mti alioupanda kati ya 600 iliyotolewa na Benki ya KCB Tanzania ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti 21,000 iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Msamvu B, Mfanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania na Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Miti TSA Morogoro wakishiriki kupanda miti 600 kwenye shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti 21,000 iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi  wa Benki ya KCB Tanzania Tawi la Morogoro akishirikiana na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Msamvu B iliyopo Morogoro mjini kuchota maji kwa ajili ya kumwagilia miti 600 waliyoipanda shuleni hapo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya benki hiyo ya kupanda miti 21,000 iliyozinduliwa hivi karibuni Chanika jijini Dar es Salaam.
------
Katika kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya miti ya asili Benki ya KCB Tanzania Tawi la Morogoro imeitikia wito huo kwa kupanda miti 1,350 yenye thamani ya shilingi Milioni 3.5/-.
 

Miti hiyo imepandwa katika shule za Msingi Kiegea, Mibulasi na Msamvu B zote za mkoani Morogoro zoezi lililoendeshwa kwa ushirikiano wa Wafanyakazi wa benki hiyo, Walimu, Wajumbe wa kamati za shule, wanafunzi, wazazi na Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis na Watendaji wa Wakala wa Mbegu za Miti TSA Morogoro.
 
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti, Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Carlos Msigwa amesema kuwa benki yake imejikita kwenye upandaji miti kutokana na baadhi ya watu kuona mazingira sio jambo la msingi kwao.
 
Msigwa amefafanua kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na kukua kwa shughuli za kibinadamu jamii isipopambana na kuidhibiti hali hiyo kwa kupanda miti na kuacha kuharibu maziungira  jangwa na maafa vitazidi kutokea.
 
“Kupanda miti katika maeneo ya shule sio tu kunalinda mazingira, bali pia kunaepusha shule kuezuliwa mapaa na vimbunga ama upepo mkali. Vilevile wanafunzi mbali ya kujipatia matunda wanaweza kujipumzisha chini ya miti kwa ajili ya kujisomea,” alisema Meneja Msigwa.
 
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya shule ya Msingi Msamvu B, Nassoro Korwe ameziomba taasisi zingine kuiga mfano huo kwa kuisaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto zingine zinazojitokeza.
Akitaja baadhi ya changamoto Mjumbe Korwa amesema licha ya Benki ya KCB Tanzania kuwapandia miti wanakabiliwa na ukosefu wa maji kwa ajili ya kumwagilia miti hiyo ili isife kwa ukame.
 
“KCB Morogoro tayari wametupandia miti, tunaomba wahisani wengine wajitokeze kutusaidia upatikanaji wa maji kwa kipindi cha mwanzoni ili wanafunzi wayatumie kumwagilia miti. Hilo lisipofanyika mchango huu wa wahisani utakuwa umepotea bure.
 
Katika hatua nyingine Kiranja mkuu wa shule hiyo Hadija Maganga ameishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema sasa watakuwa katika mazingira safi na salama kwa ajili yak masomo.
 
Mbali na hilo alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa benki hiyo kuangalia namna ya kuisaidia shule hiyo madawati ili kukabiliana na tatizo la baadhi ya wanafunzi kubanana ama kukaa kutokana na upungufu wa vifaa hivyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages