Benki ya Barclays ya Tanzania, imetangaza kuanzisha mpango wake wa harambee unaoitwa Step Ahead. Kwa kusaidiana na Washirika wengine, Benki hii itaendesha zoezi la ukusanyaji wa fedha, kusaidia kutoa huduma ya afya kwa vichanga na mama wajawazito.
Hii Step Ahead
ni ya pili kwa mpango huu unaosimamiwa na Benki ya Barclays Tanzania.
Hatua ya kwanza ya mpango huu ilifanyika mwaka 2008, na michango yote
ilikuwa kusaidia Taasisi ya saratani ya Ocean Road.
“Tumeweka lengo la makusudi, na tunategemea kukamilisha mengi zaidi mwaka huu,” amesema Afisa Mahusiano wa makao makuu ya Benki ya Barclays Tanzania, Kati Kerenge.
Fedha
hizo zitakusanywa kupitia mpango mkakati wa ushirikiano na Mashirika
mengine ambayo yataombwa kufadhili au kuchangia mpango huo kwa njia ya
kuuza tiketi. Kilele cha tamasha hilo kitakuwa tarehe 10, ya mwezi
Septemba mwaka huu wa 2011, wakati kutakapokuwa na matembezi ya kilometa
10 na kukimbia kilometa 5 ya Family Bazaar pamoja na tamasha la muziki,
litakalowahusisha Wasanii wa ndani katika kuunga mkono tukio hilo.
Kwa Habari Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)