Mtandao
wa kigaidi wa al Qaeda, umemtangaza Ayman al-Zawahiri kuwa ni kiongozi
wao mpya, baada ya kuuawa kwa Osama bin Laden na kikosi maalumu cha
jeshi cha Marekani mapema mwezi uliopita.
Tangazo hilo limetolewa katika mtandao wa itikadi kali za kiislamu. Zawahiri alikuwa kiongozi namba mbili wa al Qaeda kwa muda mrefu.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo, mtandao huo pia umesema kwamba utaendelea na vita vyake vitakatifu dhidi ya Marekani na Israel.
Wakati huohuo, mahakama katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta imemhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani mfuasi wa kundi la wenye misimamo mikali ya kiislamu Abu Bakar Bashir baada ya kumtia hatiani na makosa ya ugaidi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)