Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa akikata utepe kuzindua huduma ya M pesa inayotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Samunge Wilaya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa (kushoto) akishuhudia wakati Mchungaji Ambilikile Mwasapila (katikati) akipokea simu ya mkononi yenye kutumia nguvu ya jua ikiwa na muda wa maongezi wa sh 50,000 toka kwa Msimamizi wa wakala wa kampuni ya vodacom kanda ya kaskazini, Michael Kasubi na msimamizi wa masoko wa vodacom kanda ya kaskazini, Riziki Mwalupindi, jana baada ya kampuni hiyo kuzindua huduma ya M pesa Samunge Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa akipokea simu ya mkononi inayotumia mwanga wa jua toka kwa msimamizi wa masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini jana, mara baada ya kuzindua huduma ya M-pesa Samunge wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
--
Wakazi na wasafiri wanaokwenda kwa Mchungaji Ambilikile Masapile, ‘Babu’ Loliondo, Mkoani Arusha , kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu sasa wanaweza kupata huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha kwa njia ya M-PESA inayotolewa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando, kampuni yake imeanza kutoa huduma hiyo mapema wiki hii na kwamba sasa wakazi wateja wa babu wanaoenda kupata huduma za kiafya hawana haja ya kutembea na fedha nyingi mifukoni mwao.
M-Pesa, ni huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha inayotolewa na Vodacom Tanzania, pia kupitia huduma hiyo, mteja wa Vodacom pia anaweza kuweka amana kwenye akaunti yake ya M-Pesa. Kupitia huduma hiyo watanzania wengi wamekuwa wakitumia sana huduma hiyo na hivyo kurahisisha maisha yao.
Amesema kuwepo kwa huduma ya M-PESA katika eneo la Loliondo kunatoa fursa kwa waananchi wanofika eneo hilo kutoka maeneo mbalimbali kuwa na urahisi wa kupokea ama kutuma fedha kwa ndugu na familia zao pindi taatioz lolote linapojiotkeza kupitia wakala mabao tayari wanapatikana.
Nguvu ameongeza kuwa pamoja na kutuma na kupokea fedha huduma ya M-PESA itatoa uslama wa fedha za watu wanaofkwenda eneo hilo kwa kuwa sasa hawatolazimika kubeba fedha njiani na kwamba wanachoweza kukifanya ni kutumia mfumo huo na kuchukua pesa kulingna na mahitaji yao wanapokuwa safarini katika eneo hilo.
Aidha mbali na wanaofika kwa ajili ya huduma za Babu huduma ya M-PESA ni ukombozi mpya kwa wakazi wa Loliondo na maeneo jirani kunufaika na huduma hiyo ambayo tayari imeonekana kuwa msaada kwa jamii hapa nchini kwa kutoa urahisi wa kutuma na kupokea fedha.
Bw. Kamando alifafanua kuwa huduma hiyo iko wazi kwa wateja wa mitandao yote na kwamba mteja wa Vodacom anachopaswa kufanya ni kupitia usajili rahisi.
Alisema huduma hiyo inapatikana kwa mawakala wa Vodacom waliopo maeneo ya Loliondo na kwamba kupitia mawakala hao wateja wa Vodacom Tanzania pamoja na wateja wa mitandao mingine wataweza kufaidika na huduma hiyo.
Ufunguzi wa huduma hiyo ya M -PESA katika eneo la Loliondo unakwenda sanjari na uzinduzi wa huduma za simu za mkononi za mtandao wa Vodacom.
“Mbali na huduma hii ya M-Pesa, wateja wa Vodacom Tanzania sasa wanaweza kufurahia mawasiliano kwa kupiga na kupokea simu kwa ubora wa hali ya juu wakiwa Loliondo kwa Babu”
Akizindua huduma hizo za Vodacom hapa Loliondo, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa aliipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kupeleka huduma hizo kwa wakazi na wageni wa eneo hilo kwa muda muafaka.
Alisema kwa kuwa eneo hilo kwa sasa lina wageni wa ndani na nje ya nchi huduma za uhakika za mawasiliano na zile za kifedha ni muhimu sana.
“Nawapongeza kwa kuanzisha huduma zenu katika eneo hili kwa wakati muafaka na hivyo kuboresha maisha ya watu walioko katika eneo hili hasa kwa huduma zenu za simu zenye uhakika na pia huduma maarufu hapa nchini ya M-Pesa,huduma ambayo inawawezesha Watanzania kutumiana pesa popote walipo,”
Baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa huduma hizo za simu na M-PESA wameipongeza Vodacom kwa kupeleka huduma zake katika eneo hilo.
“Tunaipongeza Vodacom kwa kutuletea huduma hii, wenzetu wengi wamepata shida hasa pale wapoishiwa fedha kwani kulikuwa hakuna njia nyingine ya utumaji wa fedha kutoka kwa ndugu na jamaa zao.Sasa kupitia M-Pesa watu wengi wenye matatizo wanaweza kupata fedha kutoka kwa jamaa zao pale wanapoishiwa fedha” alisema Juma Sudi mkazi wa Tabora.
Kabla ya kuzinduliwa kwa huduma ya M-PESA katika eneo la Loliondo kwa Babu kumekuwepo na kero kubwa kwa wanaofika katika eno hilo kuishiwa fedha na kukosa njia bora za uhakika na salama za kupata fedha jambo ambalo limekuwa likiwalazimu watukuuza vifaa vyao ikkwemo simu za mkononi ili kupata fedha za kujikimuikiwemo wanapopata na dharura .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)