SHINDANO LA JENGA NCHI YAKO LAJA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHINDANO LA JENGA NCHI YAKO LAJA

Shindano litakalojulikana kwa jina la Jenga Nchi Yako, maalumu kwa ajili ya kusaka wasanii wenye vipaji kutoka vijiweni waishio jijini Dar es Salaam, linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni chini ya mpango wa kuhamasisha vijana kuachana na  vitendo vya uhalifu na kujiajiri kupitia vipaji vyao.

Akizungumza na Gazeti hili jana (Alhamisi) Balozi wa Amani na Ulinzi Shirikishi Vijana Taifa, Richard Manyota, ambaye ni muandaaji wa shindano hilo alisema uamuzi wa kufanya hivyo umetokana na ndoto zake za kuwaunganisha vijana nchini ili kupambana na changamoto za kimaisha.

“Mimi na wenzangu kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers tumeona tufanye shindano, tutafute vijana kutoka wilaya tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni ambao wataunda kundi la muziki wa Kizazi Kipya,” alisema Manyota.

Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa kundi hilo yeye kwa kushirikiana na mdhamini watalipeleka studio kurekodi wimbo na baadaye kulisaidia katika promosheni za utambulisho ili liweze kujulikana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages