Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto)akisikiliza maelezo ya Elizabeth Mlay, mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam, jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama.
Brighton Jacob, mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari Kiluvya iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutambua aina mbalimbali za udongo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, akiangalia aina mbalimbali ya vitabu vya kufundishia somo la kemia wakati wa ufunguzi wa mwaka wa kimataifa wa kemia.
Kakue Mafole kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali (kulia) akiwaelezea waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na waziri wa ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa (wapili kushoto) jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi za kupima vitu mbalimbali.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)