RIDHIWANI KIKWETE: MIMI SIO BILIONEA WANANISINGIZIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RIDHIWANI KIKWETE: MIMI SIO BILIONEA WANANISINGIZIA


Ridhiwani Kikwete
-- 

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, amesema yeye sio bilionea na kwamba wanaomtuhumu amewapa siku saba kuanzia leo, kumwombe radhi vinginevyo atachukua hatua za kisheria dhidi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ridwiwani alitaja mali anazomiliki kuwa, ni shamba lililoko mjini Bagamoyo, lenye ukubwa wa ekari 1.5, gari ndogo aina ya Toyota Camry na akaunti kwenye benki za CRDB, Stanbic na NBC.

Mkutano huo umekuja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, kumtuhumu Ridhiwani kuwa ni kijana bilionea, huku Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akipigilia msumari kuwa mtoto huyo wa rais ni tajiri anayemiliki malori, kampuni za ujenzi wa barabara, ardhi  na maghorofa ya kupangisha.

“Habari hizo zimejaa uongo, ambao madhumuni yake ni kunichafua mimi na mzazi wangu (Rais Kikwete), pia wanajaribu kupandikiza chuki ili tuonekane sisi ni wabaya mbele ya jamii, nataka waniombe radhi vinginevyo nitachukua hatua za kisheria,” alisema Ridhiwani na kuongeza:

“Mtikila na Slaa ni watu wazima, mimi sina kinga yoyote kisheria wathibitishe ubilionea wangu ili niweze kuchukuliwa hatua za kisheria 
 
“Nina shamba wilayani Bagamoyo lenye ukubwa wa ekari moja na nusu na gari aina ya Toyota Camry, sina maghorofa, sina malori, sina chochote zaidi ya hivyo nilivyovitaja. Kwa Habari Zaidi 
Bofya na Endelea.....>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages