MWENYEKITI WA TA ATEMBELEA KAMPUNI YA COMPUTER FOR AFRICA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWENYEKITI WA TA ATEMBELEA KAMPUNI YA COMPUTER FOR AFRICA


Mwenyekiti wa Tanzania Assocciation Uk Dr Lusingi akifanya ziara ya kutembelea Watanzania wafanyao shughuli mbalimbali hapa England. Dr Lusingu alifuatana na Mjumbe wa NEC Bi Asha Baraka ili naye ajionee na kujifunza wayafanyayo Watanzania hapa Uingereza . Kampuni hii ya Computer 4 Africa  inamilikiwa na mjasirimali wa Kitanzaniana aitwae Bw Aseri Katanga.Kampuni hii inajishughulisha na ukusanyaji wa kompyuta zilizotumika, kisha wanazi karabati kuziweka kwenye hali ya kuwa mpya, halafu wanazisambaza  katika nchi za Afrika nzima. Kompyuta hizi hupelekwa kwenye mashule, taasisi mbalmbali na idara za serikali. Kwa upande wa Tanzania zaidi ya shule 100 zimesha faidika na mpango huu.Katika picha juu ni mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akiteta jambo fulani pamoja na wafanyakazi wa computer 4 Africa na Mwenyekiti wa Tanz UK.

Picha ya pamoja kati ya  wakurengenzi na wafanyakazi wa Computer 4 Africa wakiwa na mwenyekiti wa Tanz Uk Dr. John Lusingu 
na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka.Kwa Msaada Wa Mjengwa Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages