Balozi wa Misri nchini Tazania Bw. Wael Adel Nasr (kulia) akimkabidhi mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema vifaa vya matibabu na dawa zenye thamani ya dola za Marekani laki tano ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 700 kusaidia huduma za afya katika hospitali ya jeshi la polisi kikosi cha Afya makao makuu (Kilwa Road)ambayo huhudumia familia za askari na wananchi leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema(katikati)akishirikiana na Kamishna wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi – CP Clodwing Mtweve na Balozi wa Misri nchini Tanzania Bw. Wael Adel Nasr (kushoto) kuimba wimbo wa Maadili ya Afisa wa Jeshi la Polisi leo wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri.
Balozi wa Misri nchini Tanzania Bw. Wael Adel Nasr akiongea na viongozi na watendaji wa jeshi la Polisi nchini wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya matibabu na dawa kusaidia huduma za afya katika hospitali ya jeshi la polisi kikosi cha Afya makao makuu (Kilwa Road) leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu vifaa vya matibabu na dawa zilizotolewa na nchi ya Misri kusaidia huduma za afya katika kituo cha afya cha Jeshi la polisi Kilwa Road, kushoto kwake ni balozi wa Misri Bw. Wael Adel Nasr.
Baadhi ya wageni, askari na maafisa wa Jeshi la Polisi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi ya Jeshi la Polisi kupokea vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri leo jijini Dar es salaam.
Kikundi cha ngoma za asili cha Jeshi la Polisi kikitoa burudani leo wakati wa hafla fupi ya ya Jeshi la Polisi kukabidhiwa vifaa vya matibabu na dawa kutoka ubalozi wa Misri nchini, tukio lililofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)