Anthony Mayunga,Tarime
SAKATA la mauaji ya wananchi wanne katika mgodi wa Nyamongo uliopo Tarime, mkoani Mara umechukua sura mpya baada ya ndugu wawili wa marehemu kudai kuwa polisi waliwapiga na kuwalazimisha kuyachoma moto majeneza waliyonunuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya mazishi.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa ndugu hao walipigwa ili wayachome majeneza hayo na kuyatumia yale yaliyonunuliwa na kukabidhiwa kwao na polisi.Mkono Bhoke ambaye ni kaka wa marehemu Chawali Bhoke, alisema tukio hilo lilitokea juzi baada ya kusimamishwa na askari polisi wakiwa njiani na majeneza hayo kuwahi mazishi.
Katika mkasa huo, Mkono alisema polisi wakiwa na bunduki, waliwalazimisha wanandugu hao kuyamwagia petroli majeneza hayo mawili na kuyateketeza kwa moto.Kama hiyo haitoshi, Mkono alidai polisi hao waliwapiga na kuwaweka mahabusu kwa muda jambo lililowafanya washindwe kuhudhuria mazishi ya ndugu zao.
Mkono aliongeza kuwa alikutwa na mkasa huo akiwa na ndugu wa marehemu Mwikabwe Mwita, mkazi wa Kijiji cha Kitunguruma."Kutokana na kadhia hiyo, ilibidi wanandugu kutumia majeneza ya polisi kuzika marehemu wao," alisema Mkono.
Hata hivyo, habari zingine zimeeleza kuwa wakati ndugu hao wakilazimishwa kutumia majeneza ya polisi kuwazika ndugu zao, ndugu wa marehemu Chacha Ngoka wa Kijiji cha Kewenja na Emmanuel Magige walizikwa kwa kutumia majeneza ya Chadema.Kwa mujibu wa habari hizo, ndugu hao jana walikuwa kwenye mikakakti ya namna ya kuwarejeshea polisi majeneza hayo, huku wakijua kwamba wenzao walikumbwa na kipigo.
RPC Boaz asema
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz alipoulizwa kuhusu matukio hayo, alisema haamini kama polisi wanaweza kufanya jambo hilo, ila akaahidi kufuatilia kwa karibu kujua kilichotokea

"Sikuwapo kazini, ila pia siamini kama polisi wamefanya hivyo. Nitafuatilia kwa karibu nijue kilichotokea," alisema
Taarifa zilizozagaa mjini Tarime zinaeleza kwamba polisi walitibua kwa makusudi mpango wa Chadema wa kufanya mkutano wa pamoja na ndugu wa marehemu siku ya mazishi kabla ya taratibu za maziko.
Juzi, wanachama kadhaa wa Chadema, Tundu Lisu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na wenzake saba walifikishwa mahakamani kwa shtaka la uchochezi.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Matena Mwikwabe alidai kuwa wananchi wamekosa imani na Serikali ya CCM kutokana mfululizo wa matukio tangu ndugu zao walipouawa.Diwani wa Kata ya Kibasuka, Suleimani Moya (CCM), alikiri kufika kwenye msiba wa Emmanuel Magige na kueleza kuwa hali kwa wapiga kura wake siyo nzuri na kuvilalamikia vyombo vya dola.
“Mimi ni diwani wa CCM, lakini kwenye ukweli nalazimika kuusema. Vifo vya watu hawa lazima halmashauri tutoe tamko, maana wanaokufa niwapiga kura wetu, kisha zinatolewa lugha zisizo nzuri,”alilalamika.
Katika hali ya kutafuta suluhu kati ya wananchi, mgodi na polisi, kesho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira amepanga kukutana na viongozi wa vijiji vya Kewanja, Nyangoto, Matongo, Genkuru, Nyamwaga, Nyakunguru na Kerende.
Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo walilithibitishia gazeti hili lakini wakasisistiza haki za wananchi lazima zipatikane.
Baadhi ya wakazi wa hapa wanaeleza kuwa tukio hilo limejenga uhasama baina ya wananchi na polisi ambao ni watu wanaopaswa kuhakikisha kuwapo kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Tamko la CUF
Katika hatua nyingine, Elizabeth Ernest anaripoti kuwa CUF imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na Jeshi la Polisi kuua raia mgodini.
Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo jana alipokuwa akisoma maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho. Alisema chama kinamtaka waziri huyo ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia ukiukwaji wa haki za binadamu kunakofanywa na jeshi hilo.
"Baraza linalaani vitendo hivyo ambavyo huripotiwa mara kwa mara kama ilivyotokea hivi karibuni katika mgodi wa North Mara. Kutokana na hali hiyo, CUF inamtaka waziri mhusika ambaye ndiye mwenye dhamana ajiuzuru kwa hili la Nyamongo," alisema Prof Lipumba.

CHANZO: MWANANCHI NEWSPAPER
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)