LEO ni Mei 21 siku ambayo Taifa linaingia kwenye kumbukumbu chungu ya kutimia miaka 15 tangu kutokea kwa ajali mbaya ya Mv Bukoba iliyochukua maisha ya Watanzania zaidi ya 300 waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza.
Mara kadhaa watu wachache walionusurika katika ajali hiyo wamekuwa wakijitokeza kutoa ushuhuda wao jinsi mambo yalivyokuwa wakati Meli hiyo ilipoinduka ikiwa inakaribia kuingia Bandari ya Mwanza.
Kitu cha ajabu ni kuwa mpaka leo serikali ya Bongo limeshindwa imeonekana bado iko usingizini katika kuweka umakini kwa vyombo vya usafiri nchini jambo linalofanya kuwepo kwa ajali za mara kwa mara zinagharimu maisha ya watanzania wengi kwa uzembe wa watu wachache.
Ni majuzi Tanzania imeshuhudia ajali mbaya ya basi katika barabara ya Moshi Arusha njia ambayo imeonekana kukosa tiba ya uzembe unaosababisha ajali za mara kwa mara.
G5click inaungana na Watanzania wote katika kumbukumbu ya tuiko hili la leo huku ikitoa wito kwa Serikali kuongea nguvu katika kushughulikia matatizo ya Barabarani yanayosabisha na mwisho wa siku kuwang’ang’ania kwa sharia kali wale wote wanaosababisha maaafa kama haya.
Habari Na Dismas Ten
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)